Familia moja iliyoishi katika chumba cha chini ya ardhi kwa miaka tisa "ikisubiri mwisho wa dunia" imepatikana na polisi nchini Uholanzi
Mwanamume wa miaka 58, na watoto wake sita walio na umri kati ya miaka 16 hadi 25 - walikuwa wakiishi katika shamba lao katika mkoa wa kaskazini wa Drenthe.
Walipatikana
baada ya kijana wake mkubwa kuenda kununua pombe katika baa moja karibu
na kijiji cha Ruinerwold, na kumfahamisha mhudumu wa baa hiyo kwamba
anataka usaidizi,Kituo cha Televisheni cha RTV kiliripoti.
Waliomuona kijana huyo wanasema alionekana kana kwamba amechanganyikiwa.
Familia yake imekuwa ikiishi kwa kujitenga ikisubiri mwisho wadunia, RTV iliripoti.
"Aliagiza
chupa tano za bia na kunywa zote. Baada ya hapo nilisema nae kidogo
ndipo alipofichua kuwa ametoroka na kwamba anaomba usaidizi... tukapiga
simu polisi," mmiliki wa baa hiyo Chris Westerbeek alikifahamisha kituo
cha RTV.
Aliongeza
kuwa: "Alikuwa na nywele ndefu, ndevu chafu,nguo zilizochakaa na
alionekana kana kwamba amechanganyikiwa. Alisema hajawahi kwenda shule
na kwamba hajawahi kunyolewa nywele kwa miaka tisa ."
"Alisema ana ndugu na dada zake ambao wanaishi katika shamba hilo. "
Maafisa
walitembelea makaazi hayo ya vijijini ili kufanya upekuzi zaidi.
Waligundua ngazi iliokuwa nyuma ya kabati katika sebule ya nyumba hiyo
ambayo inaelekea chumba cha chini ya ardhi ambako familia hiyo ilikuwa
ikiishi.
Polisi
imethibitisha mjini Drenthe kuwa mwanamume huyo wa miaka 58 amekamatwa
na kuongeza anafanyiwa uchunguzi-baada ya kukataa kushirikiana nao.