SITAKUSAHAU... Angel sehemu ya sita

Admin
By -
0

Nitakupeleka kwa rafiki yangu mmoja anaitwa Stanley ni raia  wa DRC ana garage yake  atakusaidia lazma utapata kazi wala usihofu Steve

Baada ya maongezi ya muda mrefu yule mtanzania akamwambia Steve twende mjini tukatembee pia na wewe uifahamu mitaa ya jiji la  Johannesburg

Wakawasha gari aina ya Ford ranger wakaanza safari ya kuelekea mjini baada ya mwendo wa kama dakika kumi wakasimamishwa na polisi SAP "South Africa Police" na wakaambiwa washuke chini  ili wakaguliwe


Kumbe polisi wa mji huwa wanamfahamu yule mtanzania kuwa ni muuzaji wa madawa ya kulevya baada ya kupekuliwa wakakutwa na gramu hamsini za cocaine kitu kilicho mshitua Steve na kujikuta ameingia katika majanga ambayo hakuyatarajia


Polisi wakawaambia waendeshe gari waende kituo cha polisi Steve akamuuliza yule mwenyeji wake kuwa "inakuwaje?" Yule mwenyeji akamjibu usiwaze kawaida hii tutaenda watatuachia

Walipofika kituo cha polisi yule mtanzania akaingizwa kwenye chumba na baada ya muda wa nusu saa  akatoka na kukwambia Steve twende tuondoke


Wakiwa njiani akamuuliza imekuwaje tumeshikwa na unga na tumeachiwa? Akamjibu hawa ukiwapa pesa kidogo Mbona wanakuachia usiwaze ndiyo tunavyoishi huku


Moyoni Steve akaanza kujutia kumfahamu huyu mtu  ambae alimpokea huku Afrika ya kusini lakini hakuwa na chakufanya kwakuwa hakuwa jinsi ikambidi avumilie...


INAENDELEA....


Mtazame hapa Mtoto mwenye kipaji cha ajabu

Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)