MTOTO WA RAISI AKUTWA AMEJIUA

Havana: MTOTO wa kiume wa kwanza wa aliyekuwa rais wa Cuba, Fidel Castro, aitwaye Fidel Ángel Castro Díaz-Balart (68) jana alikutwa amejiua mjini Havana, mji mkuu wa nchi hiyo. Castro Díaz-Balart aliyefahamika  kama “Fidelito”  alidaiwa na madaktari alikuwa ana matatizo ya msongo wa mawazo.


Castro alikuwa  mshauri wa kisayansi wa Baraza la Serikali ya Cuba na alifanya kazi kama Makamu wa Rais wa Chuo cha Sayansi cha Cuba, pia alifanya kazi kama mwanafizikia ya nyuklia.

Gazeti rasmi la Serikali ya Cuba la Granma limeripoti kuwa; “Fidel Castro Diaz-Balart, aliyekuwa akitibiwa na kundi la madaktari kwa miezi kadhaa kutokana na msongo wa mawazo, alijitoa uhai asubuhi hii, (jana).”

Televisheni ya taifa ya nchi hiyo imesema amekuwa akipokea matibabu kwa miezi ya karibuni kama mgonjwa wa kutibiwa na kurudi nyumbani, baada ya kulazwa hospitalini kwa muda.

Baba yake, Mzee Fidel, alifariki November 2016 akiwa na umri wa miaka 90 baada ya kuugua kwa muda mrefu.


Post a Comment

Previous Post Next Post