SIMBA YATOA LIST KAMILI WALIO TEMWA NA WALIO SAJILIWA

Tumesikia mengi katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili kwamba klabu ya Simba imepanga kupiga panga baadhi ya wachezaji na kusajili wengine wapya.

Wanaotajwa kupigwa chini ni pamoja na mshambuliaji wa kimataifa kutoka Burundi Laudit Mavugo, mghana Nicholas Gyan na nahodha wao mzimbabwe Method Mwanjale.

Mwenyekiti wa usajili wa klabu hiyo Zacharia Hans Poppe amesema, katika kipindi hiki ni mchezaji mmoja tu ambaye ataachwa ambaye ni Method Mwanjale.



“Ninavyoelewa mimi, mchezaji ambaye ataachwa ni Mwanjale peke yake lakini hakuna mwingine anayeachwa wala hakuna mwingine anayeongezwa zaidi ya huyu (Asante Kwasi) kama tutampata.”

Kauli hiyo kauli hiyo ya Hans Poppe inafunga mijadala ya nani na nani wataachwa wala wale ambao watasajili katika dirisha dogo, hivyo Mavugo na Gyan bado wapowapo sana Simba.




Post a Comment

Previous Post Next Post