Katika kuazimisha miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania bara Rais wa Tanzania Dk John Magufuli kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo amewasamehe wafungwa 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa.
Kivutia uwanjani hapo kwa maelfu waliofurika katika Uwanza wa Uhuru, Mjini Dodoma ulifurika kwa shangwe baada ya Rais Magufuli Kutangaza kumwachia huru Mwanamziki nguli wa Tanzania Nguza Viking maarufu kwa Jina la Babu Seya na Mtoto wake Johnson Ving au Papii Kingi
Mwanamziki huyo alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa miaka kadhaa iliopita
Hata hivyo idadi ya wafungwa wengine walioachiwa huru kutokana na makossa mbali mbali ni 1,821 ambao amesema kuwa wanapaswa kuachiwa mara baada ya tangazo lake.
Wafungwa wengine 8157 wamepunguziwa adhabu zao. Idadi hiyo ya msamaha kwa wafungwa inatajwa kuwa ni kubwa katika awamu zote kuwahi kutokea na hasa zinazo wahusisha wafungwa wa kunyongwa na vifungo vya maisha
Tags
Kitaifa