Aliyekuwa kocha wa Simba Joseph Omog, amesema alijua kama atafukuzwa kuifundisha klabu hiyo tangu mwanzoni mwa msimu huu ndiyo maana alikubali kirahisi maombi ya kuvunja mkataba na viongozi wa klabu hiyo.
Omog ameiambia Goal, Simba inamatatizo makubwa ndani yake ingawa mashabiki na watu wengine wanaiona kuwa ni timu bora kwa sasa yenye kustahili kushinda kila mchezo jambo ambalo siyo kweli.
“Simba inamatatizo makubwa ambayo siwezi kuyasema hadharani kwasababu wanaweza kuvurugana na kupoteza marali kwa wachezaji na kufanya vibaya kwenye ligi na michuano mingine ya kimataifa, lakini wanapaswa kutulia na kumaliza tofauti zao ili timu iweze kufanya vizur,” amesema Omog raia wa Cameroon.
Kocha huyo amesema hakushangaa kuona Jackosn Mayanja akiondoka kwasababu ni kocha ambaye muda mrefu aliyaona matatizo yanayoitafuna timu hiyo ndiyo maana aliamua kujiweka pembeni akisingizia ana matatizo ya kifamilia.
Amesema anaondoka Simba, lakini anajivunia kuiacha timu hiyo kwenye nafasi ya kwanza katika ligi na kusajili kikosi bora ambacho licha ya kuanza taratibu lakini amekitabiria ubingwa msimu huu endapo viongozi hawatowachanganya wachezaji
Post a Comment
0Comments
3/related/default