WAZIRI WA FEDHA WA ZIMBABWE AKAMATWA
By -
November 25, 2017
0
Harare, Zimbabwe. Waziri wa fedha katika serikali ya Robert Mugabe iliyoondolewa wiki hii, Ignatius Chombo, amefikishwa kortini Jumamosi kujibu mashtaka ya rushwa, mwanasheria wake Lovemore Madhuku amesema.
Chombo alikuwa mmoja wa mawaziri waliokamatwa na Jeshi lilipofanya mapinduzi baridi na Ijumaa alilazwa hospitalini kutibiwa majeraha aliyopata kutokana na kipigo alichopata alipokuwa kizuizini tangu Jumatano ya wiki iliyopita.
Madhuku amesema Chombo alipata majeraha kwenye mikono, miguu na mgongo na wiki nzima alipokuwa kizuizini alikuwa amefungwa kitambaa usoni.
Mashtaka yanayomkabili ni ya ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka alipokuwa waziri wa serikali za mitaa zaidi ya muongo mmoja uliopita. “Ulikuwa ukatili na unyama mkubwa wa namna ya kukabiliana na wapinzani,” limeandika shirika la habari la Reuters.
Tags: