WATUMISHI WA UMMA KUPANDISHIWA MISHAHARA MWEZI HUU





Kilio cha muda mrefu cha watumishi wa umma kitatoweka mwezii hu baada ya  serikali kuahidi kupandisha mishahara yao, taarisa zimeeleza.
hayo yamesemwa leo na , Mkurugenzi Mkuu wa Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk Hassan Abbas wakati akizungumza katika kipindi cha 360 kinachorushwa na kituo cha runinga cha Clouds TV leo asubuhi.
Akizungumzia miaka miwili ya uongozi wa Rais John Magufuli  Dk Abbasi amesema kuwa nyongeza hiyo itaonekana kwenye mishahara ya watumishi kuanzi mwezi huu baada ya kufanyika uhakiki wa veti na wafanyakazi hewa. 
“Baadhi wameshaanza kupewa barua na maofisa utumishi kama huna mazoea ya kusalimia ofisi ya afisa utumishi wewe pita pita tu pale,” Amesma Dk Abbas
Mkurugenzi huyo amesema kuwa baada ya serikali kushughulikia wafanyakazi hewa, imeweza kuokoa Sh238bn na wafanyakazi wenye vyeti ‘feki’ Sh142bn. Jumla ya Sh380bn kimeweza kuokolewa baada ya kufanyika uhakiki wa watumishi hewa na vyeti.


Hata hivyo, msemaji huyo ameeleza kuwa fedha ambazo zimepatikana baada ya kudhibiti ubadhirifu na kuongezeka kwa mapato serikali hadi kufikia Sh14trn kwa mwaka yameiwezesha serikali kutoa elimu bure, kuboresha huduma za afya pamoja na kugharamia miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo miundombinu ya usafirishaji na maji.

Post a Comment

Previous Post Next Post