Asubuhi hii tumekusogezea habari kubwa kutoka kunako klabu ya simba ambapo habari ya Kwanza ni hii hapa.
Taarifa kwa vyombo vya habari.
Klabu ya Simba inapenda kuwatangazia kuwa leo siku ya Ijumaa tarehe 1/12/2017 itakuwa na mkutano na vyombo vya habari.
Mkutano huo utafanyika kwenye ukumbi mdogo wa klabu kuanzia majira ya saa tano kamili asubuhi.
Katika mkutano huu,mambo mengi ya umuhimu yatawekwa wazi kwenu ili mtusaidie kuyafikisha kwa wanachama na wapenzi wa klabu yetu.
Tunaamini mtazingatia na kujali muda uliowekwa kwa mkutano huo kuanza.
Habari Nyingine ni kuhusu kurejea dimba kwa klabu hiyo ambapo baada ya mapumziko ya kupisha michuano ya CECAFA Simba inatarajiwa kuanza mazoezi ya kujiandaa na mchezo ujao wa ligi kuu Tanzania dhidi ya Ndanda Fc.
Kikosi cha Simba kinatarajiwa kurejea mazoezini Jumatatu baada ya mapumziko ya siku saba.
Simba itakuwa inajiandaa na mchezo utakaofuata ambapo itakuwa mgeni wa Ndanda FC kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.
Habari ya Tatu asubuhi hii ni kuhusiana na kurejea kwa straika machachali na kinara wa magoli ligi kuu Tanzania bara,Emmanuel Okwi baada ya kukosekana uwanjani kwa majuma kadhaa.
Taarifa zinaeleza kwamba mchezaji huyo anatarajiwa kuanza mazoezi na wenzake siku ya jumatatu katika mazoezi yatakao wakosa nyota wote walioitwa katika timu zao za taifa

Tags
Michezo