MWANACHAMA WA CHADEMA ATEKWA MKOANI IRINGA

Admin
By -
0
Mbunge wa Iringa Mjini  Peter Msigwa amethibitisha kuchukuliwa na Mwanachadema (Linus) wa Iringa na watu wasiojulikana waliokuwa na silaha za moto.

Msigwa amesema kwamba watu hao wamefika katika ngome yaoya kuratibu Kampeni za uchaguzi wa udiwani wakiwa na aliyekuwa diwani wa CHADEMA na kisha kuhamia CCM (ambaye ni mgombea tena wa nafasi hiyo kwa sasa) ambapo yeye ndiye amekuwa akionyesha watu wa kukamatwa.
Ameongeza kwamba kwakutumia  juhudi zao binafsi imewabidi kuwasiliana na OCD pamoja na afisa upelelezi wa wa wilaya kuhusu kuvamiwa kwa watu wao ikiwa ni pamoja na kwenda kwenye vituo vya polisi kwa ajili ya kuweza kufuatilia wapi mtu wao alipopelekwa.
"Kuna watu nimewatuma waende polisi kwa ajili ya kuwafatilia kama amepelekwa. Nimewasiliana na OCD ingawa ameniambia yupo kwenye ziara ya Kikwete, pia Afisa upelelezi wa wilaya na tayari kituo cha polisi tumepeleka namba ya gari moja ambalo lilionekana kwenye uvamizi huo" Msigwa.
Akizungumza kuhusu watu waliodhurika kutokana na tukio hilo Msigwa amesema kwamba "Watu walishakusanyika kwa ajili ya kuwazingira watu hao waliovamia  lakini walipoonyesha bastola zao watu wakarudi nyuma. Kwa kifupi CCM Kitwiru hawana namba sasa wanajaribu ku-'force'".
Sambamba na hayo  Msigwa amesema kwamba tangu jana walikwishamlalamikia RPC  kutokana na vitendo ambavyo vimekuwa vikifanywa na askari wa Mkoa ikiwa ni pamoja na kuwatengenezea watu wa Chadema kesi ambazo hazina ukweli na mpaka leo wengine wakiendelea kusota chini ya ulinzi kwa wiki nzima .
Aidha Mbunge Msigwa amesema kwamba kuna askari ambao ni wa Mkoa kutoka kwa RPC  wamekuwa wakivalia nguo za CCM zile 'Green Guard'  kwakushirikiana na vijana wa 'Green Guard' na kisha kuanza kuwasumbua na kuwatisha Wenyeviti wa Mtaa (Chadema) na wakati mwingine wamekuwa wakiwapiga wanachadema mawe lakini RPC mpaka sasa hajawachukulia hatua yoyote.
Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)