Jaffo ametoa kauli hiyo leo wakati akifungua semina ya siku tatu ya uwazi na uwajibikaji kwa viongozi waandamizi wa mamlaka za serikali za mitaa inayofanyika mjini Dodoma liyoandaliwa na wadau mbalimbali nchin.
Amesema kipindi cha nyuma suala la ukusanyaji wa mapato lilikuwa na changamoto kubwa sana na hasa katika kutumia mifumo ya kizamani lakini baada ya wataalamu kuleta maarifa mbalimbali hasa kutumia mifumo ya kielektroniki.
“Sehemu zingine zamani ambapo watu walikuwa wanakusanya kitengo hicho hicho wastani wa mlioni nne kwa mwezi, leo hii baada ya kuweka mifumo ukusanyaj unaazia miloni 30 na kuendelea, mfano eneo la afya zamani katika hospitali zetu tulikuwa tunatumia risiti za kawaida, mhasibu mmoja ana vitabu vyake, kitabu cha serkali kimoja lakini vyake ameprint vitatu,” amesema Jaffo.