KIONGOZI WA UPINZANI AHUKUMIWA MIAKA 25 JELA

Shirika la Haki za Binadamu la Amnesty International, limeikosoa Mahakama ya Kijeshi nchini Cameroon kwa kumhukumu kiongozi mmoja wa upinzani miaka 25 jela kwa makosa ya kuchochea uasi.

Aboubakar Siddiki kiongozi wa chama cha upinzani kaskazini mwa nchi , ndiye mwanasiasa aliyefungwa jela katika harakati za Cameroon za kuuzima upinzani hivi karibuni.

Amnesty imedai kuwa, hakuna ushahidi uliotolewa mahakamani hapo kuchangia hukumu hiyo ya mwanasiasa huyo kufungwa miaka 25 jela.

Aboubakar Siddiki alikamatwa mwaka 2014 baada ya kulaumiwa kwa kupanga kuipindua serikali ya Rais Paul Biya ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1982 na wakosoaji wake wanamtaja kuwa dikteta.

   


Post a Comment

Previous Post Next Post