Aliyekuwa makamu wa rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ameapishwa kuwa rais hii leo. Sherehe hiyo itaandaliwa katika uwanja wa kitaifa wa michezo katika mji mkuu, Harare.
![]() |
Rais mpya wa Zimbabwe- Bw. Emmerson Mnangagwa |
Mnangagwa ambaye ana umri wa miaka 75 alikimbilia Afrika Kusini wiki mbili zilizopita na akarejea nyumbani siku ya Jumatano baada ya Robert Mugabe kutangaza kujiuzulu wadhifa wa rais.
Vyombo vya habari vya serikali vimeashiria kuwa rais huyo wa zamani huenda akahudhuria sherehe hiyo na kuandaliwa gwaride la mwisho la heshima.
Kulikuwa na ripoti kadhaa jana Alhamisi kuwa Mugabe na mkewe Grace wangehudhuria sherehe hizo lakini Rais huo alioingoza Zimbabwe Kwa mkono wa Chuma hakuhudhuria.
Upinzani unamtaka Bwana Mnangagwa, ambae amekuwa mmoja wa watawala kumaliza "utamaduni wa ufisadi". Taarifa ya kuondoka madarakani kwa Mugabe mwenye umri wa miaka 93 hapo siku ya Jumanne iliibua sherehe kubwa kote nchini Zimbabwe
Makamu huyo wa zamani wa rais ambaye alirejea kutoka uhamishoni Jumatano -ataapishwa kaka uwanja michezo wa Harare.
Kufutwa kwake kazi mwezi huu kulipelekea chama tawala cha Zanu-PF na jeshi kuingilia kati na kumlazimisha Mugabe ang'atuke .