BLUE PEARL HOTEL YAFUNGWA BAADA YA KUDAIWA



Dar es Salaam. Kampuni ya Udalali ya Yono imeifunga Hotel ya Blue Pearl  kwa kudaiwa kodi na Ubungo Plaza.

Shughuli ya kufunga hotel hiyo imefanyika leo Novemba  9 asubuhi saa 12 huku wateja waliokuwa bado wamelala wakilazimika kuamshwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Scholastika Kevela amesema hotel hiyo inadaiwa kodi ya pango na Ubungo Plaza Sh.5.7 bilioni.

"Tunafunga na kukabidhi kwa mmiliki na shughuli hapa hazitaendelea tena hadi awe amelipa kodi," amesema Kevela

Mmoja wa wateja, Masoud Masoud akiwa na familia yake amesema''nimetoa hela nyingi na ilikuwa nikae kama wiki mbili na nimeingia jana, huu ni usumbufu."



ULIPITWA NA HII.? TAZAMA MAPOKEZI YA TIMU YA YANGA



Post a Comment

Previous Post Next Post