AFISA WA TRA ANAEDAIWA KUISHI "MAISHA YA PARADISO" KUPANDISHWA KIZIMBAMI DESEMABA 6


Afisa wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA),Bi. Jennifer Mushi anayedaiwa kuishi maisha ya Kifahari atapandishwa kizima Desemba 6 mwaka huu kusomewa maelezo ya awali katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

 Mshitakiwa anakabiliwa na mashitaka mawaili likiwemo la kumiliki magari 19 mali ambazo hailingani na kipato chake halali.

Katika shitaka lingine mshtakiwa anadaiwa kuishi maisha ya kifahari ya thamani ya sh. 333.255 milioni.
 Awali mshtakiwa alitakiwa kusomewa mashtaka leo Novemba 7, lakin Wakili Mkuu wa Merikali Vitalis Peter hawajamaliza kuyandaa.

Wakili huyo aliomba mahakama kupanga tarehe nyingine kitu ambacho hakikupingwa na upande wa utetezi uliowakilishwa na wakili Eliasaria Mosha
.
 Bi. Jennifer anashtakiwa chini ya kifungu cha sheria 27,(1) (a) na (b) cha Sheria ya Kuzuia na  Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Alidai kuwa kati ya March 21, 2016 na June 30, 2016 katika maeneo tofauti ya Jiji la Dar es Salaam, akiwa mwajiriwa wa TRA, kama Afisa Msaidizi wa Forodha alikutwa akimiliki mali zisizolingana na kipato chake, kinyume na sheria.

Bi. Jennifer inadaiwa alikutwa akimiliki magari 19 ambayo ni Toyota RAV4, Toyota Dyna Truck, Toyota Vitz, Suzuki Carry,Toyota Ipsum, Toyota Wish,Toyota Mark ll, Toyota Regiusage, Toyota Estima, Toyota Alex, Toyota Noah, Toyota Crown, Toyota Hiace, Toyota Estima, Toyota Lasso, Suzuki Carry, ambayo yana thamani ya Tsh. Milioni 197.6.
Mshtakiwa aliyekana mashtaka hayo yuko nje kwa dhamana

Post a Comment

Previous Post Next Post