KATIBU MKUU MPYA WIZARA YA HABARI ATAHADHARISHA MITANDAO YA KIJAMII


Image result for picha za Susan Mlawi

Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Suzan Mlawi (pichani kushoto) ameitaka mitandao ya kijamii kutoandika habari zenye chuki na uchochezi ijikite kuandika habri ze tija.

Bi. Mlawi amesema hayo leo  Ijumaa Oktoba, 27 Ikuku jijini Dar es Salaam, mara tu baada ya hafla ya kuapishwa viongozi mbali mbali walioteuliwa na Raisi jana.

" Mitandao ya kijamii ina nguvu na inachukua nafasi kubwa saana, sasa inatakiwa ijikite kuandika habari zenye tija na maendeleo kuliko kuandika habari za chuki na uchochezi." amesema Bi. Malawi

Aidha, Katibu Mkuu huyo amesema kuwa yuko tayari kujifunza kupitia vyombo vya habari na kuangalia changamoto za vyombo vya habari ili kuzitatua.

Nyie wanahabari mmebobea na ni wataalam wa masuala ya habari, niko tayari kujifunza na kuangalia tutafanye ili kuleta tija," amesisitiza  Katibu mkuu.
Awali Bi Suzan alikuw Naibu katibu Mkuu Utumishi.

Wakati huo huo aliekuwa katibu mkuu wa wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel amewaaga wafanyakazi wa wizara hiyo leo mjini Dodoma.

 Prof. Gabriel amewashukuru wafanya kazi kwa ushirikiano waliompatia wakatia anaiongoza wizara hiyo.
Kwa sasa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inaongozwa na Katibu Mkuu Bi. Suzan Paulo Mlawi na Naibu Katibu Mkuu ni Bw. Nicholous B. William



Post a Comment

Previous Post Next Post