FARU NDUGAI "PASUA KICHWA" NGORONGORO

Image result for picha za Faru Ngorongoro akiwa amekasirikaImage result for makundi ya faru
Mnyama faru aliyepewa jina la Spika wa Bunge, Job Ndugai ameanza vurugu katika Hifadhi ya Ngorongoro hususan ndani ya kreta.
Faru huyo alipewa jina la Spika Ndugai aliwahi kuwa Mhifadhi na Mjumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA).
Hayo yamesemwa na Meneja  wa Kitengo cha Wanyamapori NCAA Bw. Hillary Mushi wakati akizungumizia hatari ya Faru huyo kutoroka ovyo kunakoweza kuangukia katika mikoni mwa Wawindaji Haramu
 “Faru wote zaidi ya 60 wanaishi ndani ya Kreta la Ngorongoro, lakini hivi karibuni ‘Faru Ndugai,’ amekuwa ni pasua kichwa, kila mara anatoroka kutoka bondeni na kupanda maeneo ya nyanda za juu za Hifadhi ya Ngorongoro na kuwapa wakati mgumu askari wanyamapori kumlinda". amesema Bw. Mushi 
Kwa mujibu wa Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Ngorongoro, Dk Freddy Manongi, vitendo vya ujangili vimedhibitiwa kwa kiasi kikubwa katika himaya yake.
Inadaiwa ushindani mkubwa na vita vya mara kwa mara ya faru dume waliomo kreta kugombea majike ndio chanzo cha Faru Ndugai kutoroka kila mara bondeni humo. Wakati huo huo, afya ya Faru Mzee kuliko wote duniani yaani ‘Faru Fausta’ ambaye yuko chini ya ulinzi maalumu katika Bonde la Ngorongoro, nayo inaendelea kuimarika baada ya mnyama huyo kupona majeraha na kurejesha nguvu ya mwili.
Naye Daktari wa Wanyamapori kutoka Hifadhi hiyo Bw. Athanas Nyakii kuwa kwa sasa ‘Fausta,’ mwenye miaka 55 amepona lakini kwa sababu ya umri mkubwa, macho yake yanakosa nguvu ya kuona vizuri ndio maana tumemweka ndani ya banda maalum ili asishambuliwe na fisi na wanayma wengine kulao nyamba.
 Awali Meneja  Mushi alieleza kuwa  walikuwa wakiagiza majani hayo kutoka Kenya kwa gharama za Sh milioni tano kwa mzigo mmoja. “Mbali na gharama za kununua haya majani kutoka shamba la ‘Lord Dalamere,’ kule Naivasha, tulilipia usafiri na vibali Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Mamlaka ya Mapato (TRA), Tume ya Mionzi (TAEC) na Idara ya Uhamiaji,” alisema Mushi.
Hapa chini ni Baadhi ya Picha za Faru wakifurahi maisha kwenye hifadhi a Ngorongoro
Image result for picha za Faru Ngorongoro akiwa amekasirikaImage result for picha za Faru Ngorongoro

Image result for picha za Faru NgorongoroImage result for makundi ya faru

Post a Comment

Previous Post Next Post