Kumekuwa na taarifa za wavuvi kuokota baadhi ya maiti ufukweni dar es salaam huku maiti hizo zisijulikane ni za kina nani
mbaya zaidi maiti hizo huwa zimefungwa kamba na kuwekwa kunako mifuko ya sandarusi
kwa mujibu wa maelezo ya wavuvi wa maeneo hayo wamesema miili hiyo siyo ya wavuvi wenzao kwa kuwa wao wanamtandao wa wavuvi kutoka mtwara mpaka tanga lakini hawajapewa taarifa za kupotea wenzao
mpaka sasa zimeokotwa maiti zaidi ya tano huku zingine zikiwa ni zawanawake ambao wamefungwa kichwani tumboni na miguuni
na nyingi ya maiti hizo zimetanguliza kichwa kwenye mfuko na miguu kuonekana kwa nje huku zingine zikiwa zimeharibika vibaya
mvuvi mmoja alisema aliishuhudia maiti moja iliyo haribika ilimpelekea ashindwe kula chakula siku nzima
baadhi ya maiti zina majeraha huku haijulikani nani kasababisha mauaji hayo na kwa nini
UTATA KUHUSU MAITI ZINAZOOKOTWA UFUKWENI DAR
By -
August 21, 2017
0
Tags: