Hospitali ya kairuki ya mjini dar es salaam yashitakiwa baada ya kusahau baadhi ya vifaa vya upasuaji tumboni mwa mgonjwa
mwanamke mmoja aliye tambulika kwa jina la Khairat omary mkazi wa dar es salaam amefungua kesi namba 184 katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu akiidai fidia hospitali hiyo
mwanamke huyo anadai fidia ya shilingi milion 155 baada ya hospitali hiyo kumsababishia matatizo
amesema mwaka jana decemba alijifungua kwenye hospitali hiyo kwa upasuaji na baadae kuruhusiwa
baada ya muda akaanza kujihisi maumivu makari tumboni na baaadae akaamua kwenda kupima akapewa tu dawa za kutuliza maumivu
baadae hali ikazidi ongezeka ndipo akaamua kwenda muhimbili ambako akapimwa akakutwa na pamba kwenye mfuko wa kizazi
madaktari kwa kuokoa maisha yake wakaamua kumtoa kizazi ili asipatwe na matatizo zaidi
lakini pia baada ya kupata tatizo hilo lilimpelekea kupata ugonjwa wa fistura na kutaka hospitali hiyo kumlipa fidia
upande wa wadaiwa umetakiwa kupeleka ushahidi wao na kesi hiyo itasomwa agosti 31 mwaka huu
HOSPITALI YASHITAKIWA BAADA YA KUSAHAU VIFAA TUMBONI MWA MGONJWA
By -
August 28, 2017
0
Tags: