
Mkuu wa wilaya ya kinondoni Ally hapi pichani aliamuru mbunge wa kawe halima mdee akamatwe na awekwe mahabusu kwa saa 48
na baada ya kusema hivyo polisi walimkamata mbunge huyo na kumpeleka kituo cha polisi oysterbay na baadae kuamishiwa Centro bila ya kupandishwa kizimbani ikiwa imesha pita masaa 24
baada ya kutafutwa na wana habari mkuu wa wilaya huyo alijivua na kusema asiulizwe yeye waulizwe polisi kuhusu swala hilo ingawa yeye ndiye aliye amuru kukamatwa
mbunge huyo alikamatwa kwakile walicho kiita kutoa lugha ya uchochezi dhidi ya raisi alipokuwa akiongea na wanahabari mjini dar es salaam kuhusiana na mimba kwa wanafunzi mashuleni
mdee aliwataka chadema kwenye halmashauri zote wanazo ziongoza kuwarudisha shule mabinti waliopata ujauzito wakiwa shuleni kwakuwa ni haki yao kusoma
kauli hii ndiyo iliyopelekea kukamatwa kwake kwakile kilichoitwa uchochezi dhidi ya raisi
lakini mpaka sasa ikiwa nizaidi ya saa 48 mbunge huyo ajapandishwa kizimbani hatua inayo zua maswali mengi
Tags
Kitaifa