MADIWANI WA CUF WALAANI KUKAMATWA KWA HALIMA MDEE

Madiwani wa chama cha CUF mkoa wa dar es salaam walaani kitendo cha kukamatwa kwa mbunge wa kawe Halima mdee

akiongea kwa niaba ya wenzake diwani wa kiwalani Mussa kafana ambae ni naibu meya wa dar es salaam amesema wamelaani vikali hatua ya kukamatwa mbunge wa kawe kwa amri ya mkuu wa wilaya ya kinondoni Ally hapi

madiwani hao wamesema nchi saizi inaelekea kubaya uhuru wa kujieleza haupo mtu ukiongea kauli ya kutofautiana na kiongozi furani unakuwa umevunja sheria hali hii siyo nzuri

Mdee alikamatwa kwa amri ya mkuu wa wilaya ya kinondoni aliye agiza awekwe lumande kwa muda wa masaa 48 kwakile alicho kiita kutoa kauli ya uchochezi kwa raisi

Mdee aliitaka chadema kuwarudisha shuleni wanafunzi watakao pata ujauzito katika halmashauri zao hatua iliyochukuliwa kama kauli ya uchochezi


Post a Comment

Previous Post Next Post