WAZEE CHADEMA WAMVAA MZEE MWINYI

Wazee kutoka chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA.wamjia juu.mh rais mstaaf mzee mwinyi kufuatia kauli yake

wazee hao wakiongozwa na katibu mkuu Roderick lutembeka wamemjia juu mzee mwinyi kufuatia kauli yake ya kusema "isingekuwa katiba raisi magufuri alitakiwa atawale milele"

wazee hao wamesema kauli hii inaweza kumfanya raisi magufuri asitake kutoka madarakani kwa kuwa hata viongozi wa nchi jirani walio badilisha katiba za nchi zao walianza kama hivi

walisema mdogo mdogo wanaweza kuja na hoja ya kubadiri katiba ili waongoze milele kama amvavyo baadhi ya nchi jirani walifanya

viongozi hao wamelani vikali lugha hiyo na kusema inaweza kupelekea ubadilishwaji wa katiba ukafanyika kama ambavyo nchi zingine wamesha kifanya

katiba ya tanzania ina mruhusu raisi kuongoza kwa mihula miwili tu na baada ya hapo anatakiwa kumwachia mwingine hali ambayo.CHADEMA wameanza kuitilia mashaka kutokana na kauli kama za mzee mwinyi


Post a Comment

Previous Post Next Post