Jumamosi ya February 22 2016 utapigwa mchezo wa Dar es Salaam Derby (Yanga vs Simba) kwenye uwanja wa taifa, mchezo huo ni wa marudiano wa ligi ya Vodacom Tanzania bara.
Mchezo wa raundi ya kwanza Yanga ilishinda kwa bao 2-0 dhidi ya Simba lakini kesho nini kitatokea? Simba italipa kisasi au Yanga itaendeleza ubabe? au timu hizo zitatoshana nguvu? Majibu ya maswali yote yatajulika baada ya dakika 90 za mchezo huo.
Kuelekea mchezo huo, leo nimepita katika mitaa ya jiji la Dar es Salaam na kushuhudia kukiwa na pilika nyingi za maandalizi kuelekea mchezo huo. Jezi zinauzwa na kununuliwa na mashabiki lakini pia wapenzi wa timu hizo wameonekana wakiwa kwenye mistari mirefu wakiwa wananunua tiketi kwa ajili ya kushuhudia pambano hilo.
Cheki mwenyewe picha hizo
Hapa jezi pale tiketi, unatoka kununua tiketi unanuna jezi kesho unaingia kwenye game umependeza
Tags
Michezo










