Louis van Gaal amekiri kwamba mashabiki wa Manchester United walikuwa sahihi kuwatolea lugha chafu baada ya kupokea kipigo cha magoli 2-1 kutoka kwa FC Midtjylland ya Denmark kwenye michuano ya EUROPA League.
Mashabiki wa United walikuwa wakiimba ‘f*****g s**t’ kwa kurudia rudia hasa baada ya pambano lao kumalizika.
Mashabiki wana haki ya kutukosoa. Ni lazima tuboreshe mchezo wetu ili mashabiki warudi tena kutupa sapoti.
‘Wanafedheheka kama ilivyo kwa upande wangu pia. Nawashukuru sana mashabiki waliotusapoti lakini tulikuwa tukitaka ushindi na tunapaswa kufanya hivyo katika uwanja wetu wa Old Trafford ili kufuzu kwa hatua inayofuata. Tunapaswa kufanya hivyo japo si rahisi.’
Tags
Michezo

