Usiku wa jana katika michuano ya klabu bingwa ulaya washindi wa pili wa michuano hiyo msimu uliopita,timu ya Juventus waliweza kutoka nyuma na kusawazisha magoli yote dhidi ya mabingwa wa ujerumani Bayern Munic katika mpambano wa kukata na shoka.
Bayern waliandika bao la kwanza mnamo dakika ya 43 kupitia Tomas Muller. Bao hilo lilidumu mpaka mapumziko.
Kipindi cha pili kilipoanza iliwachukua bayern dakika 10 tu kwani mnamo dakika ya 55 Arjen Roben aliandika bao la pili.
Huku Juventus ikionekana kama ishapoteza mechi hiyo,katika dakika ya 63 Dybala aliweza kufunga goli la kwanza lililowapa ahueni mabingwa hao wa Italia.
Alikua ni Stuaro alieweza kuweka ubao wa magoli usomeka 2-2 baada ya kuipatia Juventus goli la Pili katika dakika ya 76.
Hadi dakika 90 zinamalizika matokeo yalibaki 2-2 na hivyo kufanya mchezo wa marudiano uonekane utakua mgumu zaidi kwa pande zote mbili.