HII HAPA SIRI YA MKOROGO WA RAY

Staa mahiri wa filamu Bongo  Vincent Kigosi maarufu kama Ray  amesema hajawahi kutumia mkorogo (kujichubua) ila Siri ya muonekano wake ni mazoezi anayofanya na kunywa maji mengi.

Akizungumza na kituo cha East Afrika Radio hivi karibuni Ray ambaye mng'aro wake  wa ngozi  umeonekana kuchukuliwa na mashabiki kama anatumia Dawa za kubadili ngozi ya mwili(mkorogo) ametoa kauli hii ikiwa ni siku chache tangu Nay wa Mitego alipomtaja kwenye "SHIKA ADABU YAKO"kuwa anatumia mkorogo.
Ray ameongeza kuwa hapo awali alikuwa na muda wa kwenda saloon kufanya Scrubing ndio maana alikuwa anaonekana mweusi lakini tangu ameanza kufanya scrubing kila wiki na kwenda saloon hali yake ikabadilika, huku akieleza pia maamuzi hayo yametokana na kujiweka tofauti mbele ya mashabiki wake ili wavutiwe nae pindi wamuonapo kideoni.

Post a Comment

Previous Post Next Post