AWAUA NDUGU ZAKE KWA KUWATILIA SUMU YA PANYA KWENYW CHAKULA

Polisi nchini Italia wamemkamata mwanamume ambaye anadaiwa kutumia sumu ya kuua panya kuwaua watu wa familia yake kwa sababu hawakuwa "wasafi".

Mattia Del Zotto, 27, analaumiwa kwa kuweka sumu kwenye chakula cha babu ya nyanya yake na cha shangazi ambao walifariki

Watu wengine watano katika familia wanaendelea kupata matibabu hospitalini.



Bw. Del Zotto alikamatwa eneo la Mozna karibu na Milan baada polisi kupata risiti kwenye kompiuta yake.

Baada ya kukamatwa alikiri kuwa alitaka kuwaadhibu watu wasio wasafi.
Mama yake aliwaambia wachunguzi kuwa hivi karibuni alikuwa amejiunga na dhehebu.

Post a Comment

0 Comments