LIVE.MAPIGANO YAANZA UPYA GAZA

Admin
By -
0


 Ndio tu adhuhuri imeingia nchini Israel na Gaza baada ya asubuhi iliyochafuka kufuatia mapigano kuanza tena saa za mapema. Haya ndiyo matukio yote muhimu kufikia sasa:

  • Mapigano yameanza tena huko Gaza baada ya kusitishwa kwa mapigano kwa muda na Hamas kufuatia siku saba za kuachiliwa kwa mateka.
  • Huko Gaza milio mikubwa ya risasi na mashambulizi mengi makubwa ya anga yameonekana na kusikika, huku makombora yakirushwa kuelekea kusini mwa Israel kutoka Ukanda wa Gaza.
  • Jeshi la Israel limeilaumu Hamas kwa kukiuka masharti ya mapatano kwa kushindwa kuwaachilia mateka wote wa kike na watoto wanaoshikiliwa huko Gaza.
  • Vilevile, Hamas imelaumu Israel kwa kuvunja makubaliano ya kusitisha mapigano, ikisema ilikuwa inazuia usambazaji wa mafuta kufika kaskazini mwa Gaza.

Watu kadhaa waripotiwa kuuawa

  • Wizara ya afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas imesema takriban watu 30 wameuawa na mashambulizi ya anga saa chache tangu mapigano kuanza tena.
  • Vipeperushi vimetupwa vikiwaonya watu mashariki mwa mji wa Khan Younis, kusini mwa mji wa kusini kuelekea Rafah, karibu na mpaka wa Misri.
  • IDF imeunda ramani mpya inayogawanya Gaza katika mamia ya kanda, ambayo inasemekana itatumika kuwaonya raia kuhusu maeneo wanayohitaji kuhama ili "kujiandaa kwa hatua inayofuata ya vita"

Mazungumzo yanaendelea na Marekani inatoa onyo

·Mazungumzo magumu ya kuanza tena kusitisha mapigano yanaendelea nchini Qatar, duru zimeiambia BBC

  • Kabla ya mapigano kuanza tena, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken aliiambia Israel kwamba inabidi kuwalinda raia kwa njia tofauti wakati huu, akisema idadi kubwa ya vifo vya raia na watu wengi kuhama makwao kaskazini mwa Gaza haiwezi kurudiwa tena kusini.
  • Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto limetahadharisha kuhusu janga la kibinadamu, isipokuwa kama usitishaji huo utaanza tena. Msemaji wa Unicef ​​katika hospitali moja kusini mwa Gaza alielezea hali hiyo kuwa ya kuogofya

Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)