Header Ads Widget

KIKOSI CHA UMOJA WA AFRIKA CHAANZA KUONDOKA DRC


 Kikosi cha jumuiya ya Afrika Mashariki EACRF kimeanza kuondoka mashariki mwa DRC.

Kikosi hicho kinakamilisha majukumu yake tarehe 8 mwezi huu baada ya jopo la marais kuidhinisha ombi la Kinshasa kulitaka kuondoka.

EACRF ilianza majukumu yake nchini DRC mwezi November mwaka 2022 baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa EAC Rais mstaafu wa Kenya, Uhuru Kenyatta kutia saini makubaliano na rais Tshishekedi ya kudumisha amani, miezi michache tu baada ya DRC kujiunga na EAC.

Kenya ambayo iliongoza kikosi hicho iliingia Goma Novemba mwaka huo na baadaye kusaidia majeshi ya Burundi na Sudan Kusini kujumuika katika kikosi hicho.

Kenya ilikuwa inadumisha amani katika kambi iliyowekwa kwenye uwanja wa ndege wa Goma, katika makao makuu ya kikosi mjini Goma, kibumba karibu na mlima Nyiragongo na Rumangabo.

Uganda ilidumisha amani katika eneo la Bunagana, Sabinyo na Tongo.

Sudan kusini ilishirikiana na Kenya kushika doria Rumangabo katika kambi ya kijeshi iliyowahi kusimamiwa na jeshi la FARDC.

Kwa sasa kikosi cha kijeshi cha SADC kinajiandaa kuingia mashariki mwa DRC baada ya marais wa jumuiya hiyo kuitikia wito wa rais Tsishekedi kudumisha amani mashariki mwa DRC na kukabiliana na wanamgambo.


Post a Comment

0 Comments