mkojo kuna manufaa.
Anasema, “Kupitia mkojo tunaondoa uchafu mwilini. Kwa hiyo hakuna msingi wa kisayansi wa kunywa mkojo taka kuwa na manufaa.”
Madhara kwa figo
Kulingana na Dkt. Andrew Thonber, unywaji wa mkojo unamaanisha kuwa unaweka taka ambayo mwili wako umeondoa ndani ya mwili wako. Kufanya hivyo kunaweza kudhuru afya yako.
"Figo husafisha damu na kuondoa uchafu na chumvi," aliambia BBC. Mkojo wa mtu mwenye afya njema ni asilimia 95 ya maji, na asilimia tano iliyobaki una kemikali kama vile potasiamu na nitrojeni, ambazo mwili unataka kutoa. Hivyo kunywa mkojo kunaweza kusababisha matatizo ya tumbo, na pia kuwa hatari kwa figo.”
Kulingana na yeye, "Watu wengi wanaamini kuwa kunywa mkojo kunaweza kutoa mwilini vitamini muhimu haraka, hakuna haja ya kufuata njia hizo hatari."