Mmiliki wa Twitter, Elon Musk ametangaza kufanya mabadiliko ya logo ya mtandao wa Twitter, kutoka alama ya ndege wa bluu mpaka alama ya X.
Musk alitangaza mabadiliko hayo jana Jumapili, Julai 24, 2023 na kueleza kuwa yataanza rasmi leo, Jumatatu.
Mabadiliko hayo ni mwendelezo wa mabadiliko makubwa ambayo Twitter inayapitia, tangu Musk alipoununua mtandao huo kwa gharama ya dola bilioni 44, Oktoba, 2023.
Maelezo ambayo amekuwa akiyatoa bilionea huyo namba moja duniani, ni kwamba anataka kuibadilisha Twitter na kuwa ‘App ya Kila Kitu’ kama ilivyo kwa WeChat ya nchini China, akimaanisha Twitter haitakuwa mtandao wa kijamii pekee bali Zaidi ya hapo.
Mkurugenzi wa Twitter, Linda Yaccarino amethibitisha mabadiliko hayo na kueleza kuwa Twitter inakwenda kuibadili dunia.
Watumiaji watakuwa na uwezo wa kuwasiliana kwa sauti, video, meseji lakini pia watakuwa na uwezo wa kufanya miamala ya fedha na huduma za kibenki. X utakuwa ni mtandao ambao utawezesha kila kitu kufanyika