Aliyekuwa mpishi wa obama afariki dunia

Admin
By -
0


 Mpishi wa kibinafsi wa rais wa zamani wa Marekani Barack Obama amefariki dunia wakati wa ajali kwenye safari ya kupiga kasia karibu na nyumba ya Obamailiyopo Massachusetts.

Tafari Campbell, 45, alifanya kazi katika Ikulu ya White House kabla ya kukaa na familia ya Obama baada ya Bw Obama kuondoka mamlakanimwaka 2016.

Siku ya Jumapili, alipotea ndani ya maji katika eneo la Edgartown Great ,kwenye bwawa la shamba la Mizabibu la Martha.

Obama na mkewe walitoa taarifa wakisifu vipaji vyake ndani na nje ya jiko.

"Tafari alikuwa sehemu pendwa ya familia yetu. Tulipokutana naye kwa mara ya kwanza, alikuwa mpishi wa mpishi hodari katika Ikulu ya White House - mbunifu na mwenye shauku ya mapishi ya chakula, na uwezo wake wa kuleta watu pamoja," Bw Obama na aliyekuwa mke wa rais wa zamani Michelle Obama walisema Jumatatu.

"Katika miaka iliyofuata, tulimfahamu kama mtu mchangamfu, mwenye furaha, na mkarimu sana ambaye alifanya maisha yetu yote kuwa angavu kidogo."

Bw Campbell alikuwa akitembelea kisiwa cha Massachusetts kutoka nyumbani kwake huko Virginia wakati alipokutana na mauti yake. Polisi wanasema familia ya Obama haikuwa nyumbani wakati wa ajali hiyo.

Msako ulianza siku ya Jumapili usiku kumtafuta "mwanaume mpiga kasia ambaye alikuwa ameingia ndani ya maji, alionekana kuhangaika kwa muda kukaa juu ya maji na kisha kuzama na hakuibuka tena," kulingana na ripoti ya polisi.

"Mpiga kasia mwingine alikuwa kwenye bwawa pamoja naye wakati huo na kumwona akizama chini ya maji," iliongeza.

Siku ya Jumatatu, mwili wake ulipatikana "takriban futi 100 (mita 30) kutoka ufuo kwenye kina cha futi nane".

Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)