Mapya Yaibuka Usajili Wa Adebayor Simba Bosi Aongea Na Championi

Admin
By -
0

 

SIMBA imekutana na ugumu wa kumpata kiungo mshambuliaji wa Klabu ya RS Berkane ya nchini Morocco ambayo imegoma kumuachia.

Adebayor ni kati ya wachezaji waliokuwa katika mipango ya muda mrefu ya Simba ya kumsajili tangu msimu uliopita.

Simba imepanga kufanya usajili mkubwa wa wachezaji watakaowafikisha hatua ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao baada ya misimu mitatu kuishia Robo.

Mmoja wa mabosi wa Simba, ameliambia Championi Jumatano kuwa kwa mara ya pili Simba wameifuata Berkane kwa ajili ya mazungumzo mapya ya kumsajili kiungo huyo ambaye amemalizana na uongozi wa Msimbazi iliyopanga kumsajili katika msimu huu.

Bosi huyo alisema kuwa katika mazungumzo hayo, Berkane imeonekana kuendelea na msimamo wake wa kumbakisha hapo licha ya kukosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

Aliongeza kuwa Berkane imekataa kumuachia kiungo huyo kwa mkopo kwenda Simba ambayo ilipeleka maombi hayo kumtaka kiungo huyo mwenye uwezo wa kufunga na kutengeneza nafasi.

“Berkane imeendelea na msimamo wake wa kiungo wao mshambuliaji Adebayor anayehitajika na Simba kwa mkopo katika msimu ujao.

“Hii ni mara ya pili kwetu kumuhitaji Adebayor kwa mkopo, tuliwasilisha maombi hayo ya kumtaka kwa mkopo katika usajili wa msimu uliopita, pia hivi karibuni tulipeleka tena maombi.

“Yeye mwenyewe mchezaji tumeshamalizana naye, lakini tatizo ni klabu yake inayommiliki kushikilia msimamo wa kukataa kumtoa kwa mkopo,” alisema bosi huyo.

Akizungumzia hilo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa timu hiyo, Salim Abdallah ‘Try Again’ alizungumzia hilo la usajili na kusema kuwa: “Tupo katika mazungumzo na baadhi ya wachezaji tutakaowasajili katika msimu ujao ambayo yapo katika hatua nzuri mara baada ya kukamilika tutaweka wazi.”

Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)