SIMULIZI SAFARI YANGU YA AFRIKA KUSINI SEHEMU YA 14

Aliinana chini kwa muda kidogo akiwa haongei chochote Kisha akaniuliza hivi hauna ujuzi wowote? Nikamjibu Mimi Ni fundi magari akashituka akauliza unasemaje? Nikamjibu kuwa Mimi Ni fundi magari

Akawa Kama amebadilika usoni Kisha akaniambia Sasa kwanini usitafute kipato halali? Hivi watu wakiju kuwa unauza unga Mimi nitaonekanaje? Ningekuwa sikupendi Leo tungeachana lakini nilikuhaidi kuto kukuacha ndyomaana nashindwa kukuacha maana nakupenda

Akaniuliza umewahi kukamatwa mala ngapi? Nikamjibu mala nne akajibu kwahiyo wewe Ni mzoefu wa kushikwa na Polisi? Nikajikuta nipo tu kimya Sina Cha kumjibu kiukweli alikuwa ananipenda Sana


Akaniambia nataka ubadili mfumo was maisha kwakuwa natamani uje kuwa mumue wangu ila hii biashara Mimi siibariki nihaici kuwa unaacha. Nikamuuliza nitaanzaje maisha mapya? Akajibu Mimi nitajua utaanzaje ila kikubwa nataka uache.

Nikamjibu sawa nipe muda wa mwezi nitakuwa nimeacha maana siwezi tu kuacha ghafla maana nishakuwa na mtandao akajibu mwezi mbali nakupa wiki mbili tu u adili maisha

Kweli nilifikiria kuacha lakini nikawa nawaza nitaanzaje kumwambia Thomas kuwa nataka kuacha kuuza unga?..... ITAENDELEA


Post a Comment

Previous Post Next Post