Nikamuuliza nimekuuzi kwa kitu gani? Akajibu nipo bize nitakueleza baadae nitakuambia umeniuzi kitu gani
Nikabaki nawaza Ni Nini kilichomuuzi? Nikawa sipati majibu jioni mida yaa saa kumi akanipigia akaniuliza Yale madawa ndani mwako unauza au wewe mtumiaji? Duh nilishituka nikabaki sijui nimjibu nini
Nikamwambia madawa gani? Au umeona unga wa ugari? Akajibu unanifanya Mimi mtoto? Mimi nayajua madawa usinizuge nijibu Tena Ni cocaine nimeiona niambie ukweli Mimi nijue
Nikamjibu baadae uje nikuambie ukweli nipomuambia hivo akaelewa akasema saambil usiku nakuja na staki unifiche kitu chochote nikamjibu sawa
Kweli muda ulipofika akaja akanipikia chakula akaandaa tukala tukakaa sebureni akaniambia Sasa niambie ukweli ikabidi tu nimueleze hali halisi iliyopelekea Mimi kuingia kwenye biashara ya madawa ya kulevya... ITAENDELEA
Tags
Simulizi
