Nikaingi chumbani lakini nikawa nachungulia nikawa namuona anaongea na SAP SAP maana yake South Africa Police wanawaita SAP baada ya kuongea nao kunakitu akawapa Kisha akarudi sebureni
Akaniita nikarudi Tena sebureni nikamuuliza Ni akinanani akahisi sikuwaona akajibu Kuna wahuni flani wanazingua sikutaka wakuone wewe
Nikamjibu tu powa lakini nikahisi pia hata Thomas atakuwa na harakati haramu ingawa Bado sikujua Ni harakati gani usiku kilamtu akaingia geto kwake tukalala
Hasubuhi akaniambia kuwa anaenda town ila atarudi sio muda kamavipi niandae chai ninywe yeye nisimuwekee nikamjibu powa lakini tukio la Jana liliniacha na mawazo kunanini
Mida ya saa Saba mchana akarudi akiwa na gari yake Aina ya Audi Ni magari ya kufahari kidogo akaingia ndani tukapiga stori Kisha akaniambia wacha nikuambie ukweli Mimi nauza madawa ya kulevya duh nikashituka akasema usishituke kawaida tu
Nikamuuliza inamaana biashara ya vifaa vya electronics Ni ya nani? Akajibu Ni yangu nazugia tu Ila biashara yangu kubwa Ni hii na nnatmani tuifanye wote
Duh nikatulia kwanza kimya nikawaza wale jamaa wa mwazo Ni wezi huyu muuza unga dah nomejikanyaga nikawaza nitaenda wapi na jamaa kanishilikisha nikikataa hatonizuru? Ikabidi nikubali baada ya kukubali akanipa masharti ya kazi.... ITAENDELEA
Tags
Simulizi
