Siku hiyo tulipanga kwenda kuiba kwenye mtaa mmoja wa matajiri unaitwa Parktown mtaa huu Ni miongoni mwa mitaa inayokaliwa na matajiri mjini Johannesburg
Mda ulipofika akaongezeka rafiki yao mmoja raia wa naijeria ambae Ni mwizo mwenzao wa muda mrefu pia ndiyo huwa anatumika Kama dereva kwaajili ya kubeba vitu kwenye gari
Tulipofika eneo la tukio ambako walipanga kwenda kuiba walikuwa wamesha chora ramani kuwa ndani ya nyumba Kuna watoto na mfanyakazi wazazi hawapo mda huo
Mimi nilipewa kazi ya kuvipokea vitu nje ya fensi wao ndiyo wanaingia kuiba na kweli baada ya wao kuingia wakanishitua kuwa nipokee chakwanza kupokea ilikuwa TV ilikuwa kubwa mno hata sikuwahi kuiona pia kulikuwa na vitu vidogo vidogo vingi Kama laptop,simu,redio na pia pes Kama Randi 200000 Ni pesa nyingi
Tukafanikiwa kuondoka lakini sikufurahia Aina ile ya maisha ya kuiba kwakuwa sikuwa na haiba na wizi. Basi maisha yetu yakawa Ni hayo kuiba na kuuza kwa muda wa miezi nane
Kunasiku niliona Kuna mtu Kama ananifatilia vile na sikumjua Ni Nani nipoona ananifatilia saana ikabidi nimuulize wewe Ni Nani? Akanijib kuwa anaitwa Thomas Ni Mtanzania kwao shinyanga sehemu inaitwa mwasele nilifurai kufahamiana nae Kisha akaniuliza unafurahia hayo maisha?
Nikamuuliza kwanini kaniuliza hivo? Akasema wale rafiki zako Ni wezi na Mimi nawajua inamaana na wewe Ni mwizi? Nikamjibu tu kuwa Mimi hata sijawai kuiba akaniuliza umeishi nao mda gani? Nikamjibu miezi nane Sasa akauliza miezi nane unaishi na wezi alafu wewe usiwe mwizi? Nikamjibu ndiyo Mimi siyo mwizi.... ITAENDELEA
Ku