SAFARI YANGU YA AFRIKA KUSINI SEHEMU YA 10


Akaniambia shariti kuu la biashara hii Ni marufuku kutumia unachokiuza maana utaharibu biashara. Sawa nikakubali yeye alikuwa anapewa mzigo na bosi wake Kisha anawapa watu wanasambaza nikiwemo na Mimi





Baada ya kunielekeza akanipa na namba za wateja wakuanza nao miongoni mwa wateja walikuwa wa south wazungu maana wengi wao wanatumia madawa ya kulevya hasa cocaine wao wanaimudu bei yake

Nikafanya biashara ile kwa muda wa miezi minne mpaka nikawa nimezoea na wateja wapya niliwapata. Kunasiku nilihaidiana na mteja tukutana nje ya supermarket moja ili nimpatie mzigo yeye alikuwa Teja wakizungu


Utaratibu wa kupeana mzigo Ni ule ule naingia Mimi chooni nauacha mzigo natoka anaingia yeye anauchukua anaacha hella Kisha Mimi naingia Tena kuchukua hela

Nikiwa sijui hili Wala lile kumbe Polisi walituwekea mtego ili watunase sijajua jamaa alinichoma au ilikuwaje. Ile Mimi naingia tu chooni na Polisi alievaa kiraia akaingia na kunikuta Nina cocaine


Nikakamatwa nikapelekwa maabusu Kisha nikapelekwa gereza la lindela Ni gereza kuu la pale Johannesburg nilipoingia gerezani nikakutana na watanzania wengi wengi wao kesi zao Ni madawa,bangi na uporaji kunammoja anaitwa majidi yeye alihukumiwa miaka 26 kwa kosa la unyang'anyi lakini yupo tu anafurahia maisha hata ajali

Kipindi nilipokamatwa Thomas alipata taarifa akaongea na boss wake ambae Mimi simjui mpaka Leo wakafanya mpango wakahonga nikatolewa gerezani


Nikarudi uraiani na biashara ya madawa ikawa inaendelea maana ilikuwa ndiyo kama kazi yangu mjini. Nilifanya biashara mpaka nikafanikuwa kupanga apartment ambayo nilikuwa nalipa kodi kwa mwezi Rand 1400 Kama shilling 300000 hivi za Tanzania.., ITAENDELEA

Post a Comment

Previous Post Next Post