Marekani yatangaza kutoa pesa kwa atakae saidia kukamatwa kiongozi was boko haramu

Marekani imetangaza zawadi ya dola za kimarekani milioni 7 kwa yeyote atakayetoa taarifa juu ya eneo alipo kiongozi wa kundi la kigaidi lililomwaga damu nchini Nigeria na nchi za jirani, Boko Haram.

Taarifa iliyotolewa kupitia ukurasa wa Twitter wa  wizara ya sheria nchini Marekani imesema,

“Wizara ya mambo ya nje nchini Marekani itatoa zawadi ya dola milioni 7 kwa mtoa taarifa itakayofanikisha kutiwa kukamatwa kwa kiongozi wa kundi la kigaidi la Boko haram, Abubakar Shekau.”

Wakati ikifahamishwa kwamba zawadi ya feza taslimu itatolewa na wizara ya mambo ya nje pia namba ya WahtsApp na anwani ya Telegram ziliwekwa wazi.

Shekau alichukua madaraka mwaka 2010 mara baada ya kifo cha muanzilishi wa kundi hilo, Muhammed Yusuf.

Abubakar Shekau anatuhumiwa kwa kushambulia maeneo ya jeshi na raia pamoja na utekaji wa wasichana wa Chilbok.

Kundi la Boko Haram lilianza kusikika tangu miaka ya 2000, na kuanzia mwaka 2009 lilianza kufanya mashambulizi makubwa ya kigaidi, ambayo mpaka hivi yamesababisha vifo vya watu zaidi ya elfu 20. Kundi hilo tangu mwaka 2015 limekuwa likitekeleza mashambulizi katika nchi jirani kama Cameroun, Chad na Niger. Katika shambulizi lililofanywa na kundi hilo katika ukanda wa ziwa Chad watu elfu 2 walipoteza maisha.

Post a Comment

Previous Post Next Post