Mtoto anapokuwa mchanga njia pekee anayoweza kuwasiliana na mama yake juu ya uhitaji wa jambo fulani au hisia fulani ya ugonjwa au maumivu huwasilisha kwa kutumia kilio, sasa mama ambaye yupo karibu na mtoto wake inatakiwa atambue mara tu anapolia.
Lakini pia wapo wazazi ambao usiku hawalali bali hukesha wakibembeleza mtoto, kwani wapo watoto wanaopenda kulala mchana, huku usiku wakitumia kuangua kilio cha hapa na pale.
Hapa chini nimekuletea sababu za kwa nini watoto hulia usiku
1. Mtoto akiwa na njaa na anahitaji chakula anaweza kulia ili kutaka shida yake itatuliwe. Lakini kwa bahati mbaya hana namna ya kukujulisha kuwa ana njaa zaidi ya kilio. Ni vyema kufahamu aina ya sauti ya kilio inayoashiria njaa. utajua hili kwa mazoea yako ya kila siku na mtoto wako. Njaa ni mojawapo ya sababu kubwa kabisa ya mtoto mchanga kulia.
2. Joto au Baridi,
Kama ilivyo kwa watu wazima,joto kali kupita kiasi au baridi inakufanya ujisikie vibaya na kutafuta jinsi ya kurekebisha kama vile kuvaa vazi zito kama kuna baridi au kuwasha feni au kiyoyozi, vivyo hivyo kwa mtoto mchanga, anahitaji kupata ubaridi kama kuna joto kali au kuvikwa nguo nzito ili apate joto kama kuna baridi, akipitia katika hali hizi mbili mojawapo ikizidi ndipop huanza kuangua kilio.
3. Uchovu na usingizi
Watoto wanalia wakiwa na usingizi. Hii inatokea mara nyingi sana. Watoto wengi wana tabia ya kulia kabla ya kulala
Kama ukifahamu mtoto analia kwasababu ya usingizi au uchovu basi muogeshe na kumweka katika mazingira ya kulala (kumlaza mtoto)
Watoto wengine wanalala vizuri wakiwa wameshikwa mikononi na kuchezeshwa badala ya kitandani.
4. Asipo bebwa na kukumbatiwa kwa muda mrefu.
Watoto wanahitaji kubebwa na kukumbatiwa. Hii ni njia yaasili ya kunesha upendo kwa binadamu huyu mdogo.
Mtoto anapokuwa amelazwa kwa muda mrefu huwa anachoka na anahitaji kumbadirisha namna ya kulala napengine kubebwa mikononi na kukumbatiwa. Sauti ya mapigo ya moyo ukimbeba kifuani kwako inamfanya ajisikie vizuri na kujiona anajaliwa.
5. Kubadilishwa nepi
Mtoto anapojisaidia katika nguo zake anajisikia vibaya na kukosa uhuru anahitaji kubadirishwa nepi, kuoshwa na kuvikwa upya
Mtoto akilia fikiria huenda amejisaidia na anahitaji kubadirisha nepi