Papa akataa wanaume waliooa kuwa ma padre

Admin
By -
0
Papa Francis amepinga kura ya kuwatawaza wanaume waliooa katika jimbo la Amazon kama njia ya kutatua tatizo la uhaba wa makasisi wa Kikatoliki.
Maaskofu waliunga mkono hatua hiyo mwaka jana, lakini uamuzi huo ulihitaji idhini ya Papa kutekelezwa.
Makasisi wa Kikatoliki wanatakiwa kuheshimu sheria ya useja isipokua katika baadhi ya matukio ya ambapo wachungaji wa Kianglikana waliooa walipojiunga na ukatoliki na kukubaliwa kuwa mapadre.
Useja huonekana kwa mtu kama njia ya kujitolea maisha yake kwa Mungu.

Unaweza pia kusoma:

Taarifa kutoka Vatcan ilisema: "Amazon inatutia Changamoto, Papa aliandika, kuyashinda matatizo makubwa nana sio kuridhishwa na suluhu ambazo zinatatua sehemu tu ya hali."
Papa alisema kuwa kuna haja kwa makasisi wanaonaoelewa hali ya Amazon na tamaduni zake kutoka ndani ya kanisa. Tunahitaji maaskofu "kuboresha sala kwa ajili ya kuombea wito wa upadre" na kuwatia moyo wale wanaotaka kuwa wamishonari "kuchagua kufanyia kazi yao katika kanda ya Amazon".
Mwezi Oktoba mwaka jana, kongamano la maaskofu wa kikatoliki(synod ya 184) ilikutana kujadili hali ya baadae ya kanisa hilo katika jimbo la Amazon. Ilidaiwa kuwa wanaume wakongwe waliooa wanapaswa kuruhusiwa kuwa mapadre.
Padri anaongoza misa katika eneo la AmazonHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBaadhi ya wanavijiji kusini mwa Marekani wanaweza kuonana na padri mara moja kwa mwaka
Hata hivyo, wanahitaji kuwa wanaume ambao wanaheshimika na zaidi watoke katika jamii za wazawa ambako wanaazimia kufanyia kazi.
Inakadiriwa kuwa takriban 85% ya vijiji katika Amazon hawawezi kufanya ibada kila wiki kutokana na ukosefu wa mabadre. Baadhi wanasemekana kuwa humuona padri mara moja kwa mwaka.
Lakini vuguvugu lenye itikadi kali za Kanisa Katoliki - hususan katika bara la Ulaya na Marekani - limezungumza kupinga wazo hilo, likidaikwamba hii inaweza kusababisha kukomeshwa kwa useja duniani.
Papa Francis awali alisema kuwa ataangalia uwezekano wa viri probati (yaani wanaume wenye imani iliyodhihirika) kufanya baadhi ya majukumu.
"Tunapaswa kufikiria ikiwa kuna uwezekano wa viri probati ," aliliambia gazeti la Ujerumani la Der Zeit.
Pia Jumatano, Papa a;itangaza kuwa ameamua kutowaruhusu wanawake kuhudumu kama viongozi wa kanisa kwa cheo cha ushemas, ambacho mtu hupewa kabla ya kutawazwa kuwa padre.
Kando na hilo alitoa wito wa kulindwa kwa mazingira katika jimbo la Amazon kutokana na umuhimu wake katika kuzuwia ongezeko la joto duniani.
"Tunadai mwisho wa kuendewa vibaya na kuharibiwa kwa mama dunia ,"alisema Papa Francis.

Kuna uhaba wa mapadri katika eneo la mashambani la AmazonHaki miliki ya pichaAFP
Image captionKuna uhaba wa mapadri katika eneo la mashambani la Amazon
'Kuangazia juu ya mabadiliko ya hali ya hewa badala ya useja'
Inaweza kuwa rahisi kufikiria kwamba uamuazi wa Papa Francis wa kutokubali ombi kutoka kwa maaskofu wa Amazon ni ushindi kwa mtangulizi wake Papa Emeritus Benedict XVI na wanaozuingatia utamaduni wa kikatoliki ambao wanamchukulia kama mtu mwenye jukumu la kuendeleza viwango vyao.
Mwezi uliopita ilibainika kuwa Benedict alichangia katika kitabu, kinachofahamika kama 'From the Depths of Our Hearts', au Kutoka katika ndani ya mioyo yetu'' kilichoandikwa na Kardinali Robert Sarah, ambazo kilieleza mara nyingi kwamba makasisi lazima wawe waseja.
Lakini wakati Papa Francis alipoulizwa kuhusu suala hilo, wakati wa mkutano na waandishi wa habari alipokua kwenye ndege kurejea Roma kutoka Panama mnamo mwezi Januari 2019, alikua wazi juu ya kile anachokipendelea. "Binafsi ," alisema "ninadhani useja ni zawadi kwa kanisa.
Ninaweza kusema kwamba sikubaliani na kuruhusu useja kuwa chaguo, hapana."

Unaweza pia kusikiliza:

Papa Francis awakemea makasisi waovu
Papa Francis pia alikua na hofu kwamba kama useja utakua ni jambo muhimu la jibu lake kwa Sinodi ya Oktoba, basi masuala mengine ya muhimu kwa kanda hayatapata fursa ya kusikilizwa. Kama alivyoandika katika ukurasa wa jibu lake , "Jimbo la Amazon linakabiliwa na mkasa wa kiikolojia'' na kwa hiyo akaamua kuzungumzia sio juu ya masuala ya ndani ya kanisa ya useja bali changamoto za nje za mabadiliko ya hali ya hewa.
Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)