TAHADHARI: Taarifa hii inazungumzia vitendo vya udhalilishaji kingono
Mwaka jana Rose Kalemba aliandika kwenye blogu akieleza namna ilivyokuwa vigumu kwake- alipobakwa akiwa na umri wa maika 14- kuiondoa video kutoka kwenye tovuti maarufu ya ngono. Watu wengi walimtafuta wakisema kuwa wanakumbwa na tatizo hilohilo hivi leo.
Muuguzi alimzuia alisimama mlangoni alipokuwa akitazama kwenye chumba cha hospitali alimokuwa Rose kisha aligeuka kumtazama
''Pole sana kwa kilichokutokea,'' alisema, sauti yake ikitetemeka. ''Binti yangu pia alibakwa.''
Rose alimuangalia muuguzi. Ni mwanamke ambaye hawezi kuwa na umri wa zaidi ya miaka 40, Rose alifikiria, binti yake anaweza kuwa mdogo kama mimi.
Alikumbuka asubuhi ile baada ya tukio la kubakwa, alikumbuka mazungumzo yake na polisi ambaye hakuonesha chembe ya huruma na daktari. Kila mtu alitumia neno ''madai'' walipokuwa wakielezea tukio lililoelezwa na Rose.
Ukiacha baba yake na Bibi yake, walezi wake wengi hawakumuamini pia.
Kwa muuguzi ilikuwa tofauti. ''Aliniamini,'' Rose alisema.
Ilikua jambo lililompa matumaini sana kwa watu kutambua kilichotokea. Ahueni ilikuwepo, ikiashiria mwanzo wa kupona.
Lakini baada ya muda mfupi maelfu ya watu wataanza kuona tukio hilo la ubakaji wao wenyewe na kwa wale ambao hawakusikitishwa na tukio hilo.
ROSE KALEMBA
Lakini basi mtu aliibuka. akiwa amemshikia kisu alimlazimisha aingie kwenye gari. Katika kiti cha abiria alikuwa mtu wa pili, mwenye umri wa miaka 19 - alikuwa anamuona mjini. Walimpeleka nyumbani kwa kando kando ya mji na wakambaka kwa muda wa saa 12, wakati mtu wa tatu alikuwa akipiga picha za video wakati wa tukio hilo.
Rose alikuwa katika mshtuko - hakuweza kupumua. Alipigwa vibaya na kuchomwa kisu kwenye mguu wake wa kushoto nguo zake zililoa damu. Alianguka na kupoteza fahamu.
Wakati fulani, mmoja wa wanaume alitoa Kompyuta mpakato na kumuonesha video Rose zilizochukuliwa wakati walipokuwa wakiwabaka wanawake wengine .
Baadaye, wanaume hao walitishia kumuua. Kwa kujilazimisha, Rose alianza kuongea nao. Ikiwa wangemwachilia, asingeweza kuwatambua, alisema. Hakuna kitu kingewatokea, hakuna mtu angejua.
walipomrudisha ndani ya gari, wanaume hao walimtupa barabarani karibu umbali wa nusu saa kutoka nyumbani kwake.
Akitembea kupitia mlango, alijiona kwenye kioo cha ukumbini . Ni mshtuko kichwani kilikuwa na damu.
Baba yake, Ron, na wana familia kadhaa walikuwa kwenye sebule karibu kula chakula cha mchana. Bado damu ikichuruzika kutoka kwenye jeraha lake alipochomwa, alielezea kile kilichomtokea.
"Baba yangu aliipigia simu polisi, alinifariji , lakini wengine walisema nimependa mwenyewe kwa kutembea usiku sana," Rose anasema.
Huko hospitalini, Rose alionwa na daktari wa kiume na afisa wa polisi wa kiume.
Afisa wa polisi wa kiume alimwuliza ikiwa tukio hilo lilianza kwa makubaliano?
Rose alishangaa. ''Nilipigwa mpaka sikujitambua.Nilichomwa kisu na kuvuja damu...''
Rose aliwaambia hapana, hayakuwepo makubaliano yoyote, alisema hakumjua aliyemshambulia. Polisi walishindwa kupata chanzo cha kuendelea na uchunguzi.
Rose alipoachiwa siku iliyofuata, alijaribu kujiua, alishindwa kujua ni namna gani angeweza kuishi maisha ya kawaida. Kaka yake alimuokoa.
ROSE KALEMBA
Miezi michache baadaye, Rose alikuwa akirambaza kwenye mtandao wa MySpace aliwakuta watu kadhaa anaosoma nao wakishirikishana anuani, kisha wakamtumia, alipoifungua ikamuonesha mtandao wa ngono, alijisikia kichefuchefu alipoona video zilizorekodiwa alipokuwa akibakwa.
Vichwa vya video hizo vilieleza yaliyokuwa yakifanyika katika video hizo, moja ikiwa imetazamwa na kutolewa maoni 400,000, Rose anaeleza.
"Video mbaya kabisa ndio zile ambazo nilizimia. Kujiona nikishambuliwa wakati ambapo sikujua ndio jambo baya zaidi.''
Hapohapo alifanya uamuzi wa kutoiambia familia yake kuhusu video hizo- wengi wa wanafamilia yake hata hivyo. Kuwaambia kusingewasaidia chochote.
Ndani ya siku kadhaa ilikuwa wazi kabisa kuwa wengi wa wanafunzi wenzake waliziona video hizo.
''Nilidhalilishwa,'' alisema ''Watu walisema nilijitakia mwenyewe. Kwamba nilikuwa malaya.''
Wavulana wengine walisema wazazi wao walikuwa wamewaambia wakae mbali naye, ikiwa atawashawishi na kisha akawatuhumu kwa ubakaji.
"Ni rahisi kwa watu kumlaumu mwathirika," anasema.
Rose anasema alituma barua pepe kwa mtandao wa Pornhub mara kadhaa kwa muda wa miezi sita mnamo 2009 ili kuomba video hizo ziondolewe
"Nilituma barua pepe kwa Pornhub nikiomba ," Tafadhali, mimi ni mtoto, hili lilikuwa shambulio, tafadhali iondoeni. "
Hakupokea jibu na video zilibaki moja kwa moja.
"Mwaka uliofuata nilijitenga," anakumbuka, "sikuhisi chochote. ilikuwa siri yangu."
Alikuwa akijiuliza kila anapokutana na watu wakamuangalia, alijiuliza kama wameona video hizo.
ngejiuliza, pamoja na kila mgeni ambaye aliangalia naye macho, ikiwa wangeona video hizo.
"Je! Walikuwa wameamua kuiona? Je! Walikuwa wamejitosheleza kwa ubakaji wangu?"
Hakuweza kuvumilia kujiangalia. Ndio sababu alifunika vioo na blanketi. Alikuwa akiosha meno yake na kunawa gizani, akifikiria wakati wote juu ya nani anaweza kutazama video hizo.
Kisha akapata wazo.
Aliandika barua pepe nyingine akijifanya mwanasheria, na kuitishia Pornhub kwa barua pepe kuwa atachukua hatua ya kisheria dhidi yao.
''Ndani ya saa 48 video zile zilitoweka.''
Miezi kadhaa baadae Rose alipata ushauri nasaha, hatimaye alieleza muonekano wa waliombaka kwa mwanasaikolojia. Lakini hakuiambia familia yake wala polisi kuhusu video.
Polisi walichukua maelezo muhimu kutoka kwa Rose na familiaa yake. Mawakili wa waliombaka walisema kuwa Rose aliridhia, na wanaume hao walishtakiwa si kwa ubakaji, bali '' kitendo chao cha kumchangia binti huyo mdogo kufanya ngono''.
Rose na familia yake hawakuwa na nguvu au rasilimali za kupambana kuhakikisha wanapata adhabu kali.

Ni wazi kabisa kuwa Ron Kalemba anafikiria sana kilichomtokea binti yake miaka yote iliyopita. Kitu gani angeweza kufanya tofauti, kama angekuwa na cha ziada cha kufanya. Binti yake alibadilika sana baada ya tukio hilo, badala ya kuwa mwanafunzi mwenye nidhamu , akawa mwanafunzi anayekosa masomo na asiyefanya mazoezi ya masomo ya shuleni anapokuwa nyumbani.
Tumekaa kwenye bustani karibu na nyumbani kwake. Yeye na Rose wakati mwinginr hukaa hapo wakisoma mistari ya biblia . Huwa hawazungumzi sana kuhusu kilichotokea nyuma.
''Inaonekana kama ulimwengu wote umemuangusha,'' anasema ''kudhalilishwa kwake, ilikuwa kama kichekesho kwa kila mtu. Imembadilisha maisha yake kabisa, na watu wanamuangusha kwa kila hatua anayoipiga kusonga mbele,''

Ron alisikia kuhusu video za mtandao wa Pornhub mwaka 2019, baada ya mtandao ambao Rose aliuelezea madhila yaliyompata habari yake kusambaa mitandaoni. Hakujua kuwa kitendo alichofanyiwa kilionekana kwa watu wengi wala hakujua kuwa alikuwa akidhihakiwa shuleni kutokana na alichokipitia.
''Nilimfahamu msichana mmoja wa darasa la nane nilipokuwa ninasoma'', Ron alikumbuka. ''Watu, walimpiga, nasi tulikaa kimya tukitazama hayo yakitendeka.''
Je anafikiria kuwa hii ndicho kilichofanyika kwa Rose?
''Ndio, lakini kwake ni mbaya zaidi. Alikuwa anakabiliwa na watu wa mitandaoni pia wakimdhalilisha. Wengine kimyakimya wengine wakimtukana. Kwake ni ulimwengu mwingine kabisa.''
ROSE KALEMBA
Katika kipindi cha miaka michache Rose alikuwa aliingia katika ulimwengu wa mitandao.
Alijiingiza kwenye kuandika, kujieleza kwenye mitandao ya kijamii na blogu mbalimbali, akitumia majina ya kubuni au wakati mwingine jina lake la kweli.
Siku moja mwaka 2019, alipokuwa akipita kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii aliona posti nyingi kuhusu pornhub. Watu wakiipongeza kwa kujitolea katika utunzaji wa wadudu, kwa ajili ya watu viziwi na kusaidia waliopitia unyanyasaji kwa kutoa usaidizi kwa wanawake kiasi cha dola 25,000 kwa wanawake wanaotaka kujiunga na mafunzo ya teknolojia.
Kwa mujibu wa Pornhub, watu bilioni 42 ilitembelea tovuti yao mwaka 2019- ongezeko la watu bilioni 8.2 kutoka mwaka uliotangulia, wastani wa watu milioni 115.
''Ni vigumu kuikosa Pornhub kama mtumiaji wa mitandao ya kijamii,'' anasema Rose. Kwa video kama yangu ambayo vichwa vya maelezo bado vipo mtandaoni, huwezi kujua kama ni kitendo cha ubakaji kimewekwa mtandaoni hapo, waathirika hawajui kuhusu hilo.
Rose alisimulia siku moja kwenye mtandao mmoja simulizi iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kubakwa kwake, na kuishutumu Pornhub kwa kufumbia macho tukio hilo mpaka pale alipojifanya kuwa mwanasheria.
Wanawake kadhaa na hata wanaume walimuandikia Rose wakisema kuwa video ambazo walipigwa wakati wanadhalilishwa kingono pia zilionekana kwenye mtandao huo.
Katika taarifa yake kwa BBC, Pornhub imesema: ''Shutma hizi mbaya zinazoeleza tukio la 2009, miaka kadhaa kabla Pornhub haijawa na mmiliki mpya, hivyo hatuna taarifa kuhusu namna gani suala hilo lilivyoshughulikiwa wakati huo. Tangu kubadilika kwa umiliki, Pornhub mara zote imekuwa ikiweka ulinzi mkali na sera linapokuja suala la kuzuia maudhui yasiyofaa na yaliyokinyume cha sheria, ikiwa ni sehemu ya wajibu wetu wa kupiga vita maudhuo ya udhalilishaji kingono kwa watoto.''
Pornhub ilipoulizwa kwanini video zenye maelezo sawa na zile zilizohusisha kisa cha kubwakwa kwa Rose zina majina kama '' binti mdogo akidhalilishwa huku akiwa usingizini'' ''binti akidhalilishwa akiwa amelewa'' ''udhalilishaji mbaya'' bado ziko kwenye mtandao wa Pornhub, Kampuni ikasema
'' Tunaruhusu kila namna ya maelezo ambayo yanafuata taratibu zetu za matumizi , kama ilivyo kwa baadhi ya watu waonavyo kuwa si sawa, kwa wengine duniani kote hilo halina shida na wote wanalindwa na na sheria ya haki ya kujieleza.''
Pornhub ilianzisha kitufe maalumu cha kutoa taarifa kuhusu maudhui yasiyofaa mwaka 2015, lakini habari kuhusu video za udhalilishaji kwenye tovuti hiyo zimeendelea kuwepo.
BBC pia ilizungumza na mwanamke mmoja aliyemtumia Rose ujumbe wa barua pepe . Video ikimuonesha akidhalilishwa iliyobaki kwa miaka kadha mtandaoni katika tovuti moja ndogo, ingawa alituma barua pepe kadhaa kwa kampuni na kuacha maoni chini ya video hiyo. Mwanamke huyo kutoka California, anasema video hiyo ilipakuliwa pia na tovuti nyingine za ngono.
Wanasheria wa tovuti hiyo waliiambia BBC kuwa wateja wao hawakuwa na habari yoyote kuhusu tukio hilo''. Kisha BBC ilitoa anuani ya video hiyo, pia picha za maoni yaliyotolewa na mama huyo akitaka iondolewe. Hatimaye video iliondolewa mtandaoni siku zilizofuata.

''Kilichomtokea Rose mwaka 2009 bado kinafanyika leo katika tovuti kadhaa za ngono -si tu Pornhub,'' anaeleza Kate Isaacs kutoka shirika la Not Your Porn, linalofanyia uchunguzi tovuti za masuala ya ngono.
''Hatuwezi kufanya chochote kuhusu ujanja unaofanywa na mitandao mingine binafsi lakini kwa mitandao mikubwa ya ngono ya kibiashara kama Pornhub wanapaswa kuwajibishwa. Hakuna sheria inayowabana''.


Rose ana matumaini na mustakabali wa maisha yake, akiwa mwanzoni mwa miaka 20 amempata mwenza wake kwa jina Robert, ambaye anasema amemsaidia kuondokana na fikra kuhusu madhila yaliyompata. Ana matumaini ya kufunga naye ndoa na kuzaa naye mtoto wa kike, na mbwa wake aitwaye Bella, aliyekuwa akimpa nguvu.
ROSE KALEMBA
''Kwa namna nyingi, nina kifungo cha maisha.'' Rose anasema ''Hata sasa ninaweza kwenda mgahawani lakini nikakutana na mtu mgeni nikawaza kuwa huenda ameiona video ile.''
Lakini hataki kuwa kimya tena, anasema Rose, '' Silaha yenye nguvu kabisa kwa mbakaji ni kukaa kimya.''
Tags
MAKALA
