Mazungumzo zaidi yanahitajika kuhusiana na gharama za usalama wa Harry na Meghan baada ya kuamua kuishi Canada, amesema waziri mkuu Justin Trudeau.
Trudeau ameongeza kuwa gharama ya ulinzi na mipango mengine inahitaji kujadiliwa.
Malkia amekubali kipindi cha mpito ambapo mwanamfalme Harry na mkewe Meghan watakuwa wakiishi Canada na Uingereza.
Amesema kwamba anaunga mkono hatua yao ya kuanza kujitegemea lakini ingekuwa vizuri zaidi iwapo wangeendelea kutekeleza majukumu yao ya kifalme kwa muda kudumu.
Katika taarifa baada ya mazungumzo yaliyofanyika Sandringham, kwenye makazi ya Malkia Norfolk, Jumatatu, uliohusisha wanamfalme waandamizi, Malkia alisema anatarajia kwamba uamuzi wa mwisho utafanyika hivi karibuni.
Pia unaweza kusoma:
Mwanamfalme Harry na Meghan walitangaza kwamba wanataka kujiondoa kama washiriki wa muda wote katika utekelezaji wa majukumu ya Kifalme na badala yake wapate muda wa kuishi Uingereza na America Kaskazini.
Lakini hatua hiyo imeibua maswali kuhusu ni nani atakayegharamia ulinzi wao.
Trudeau amesema raia wengi wa Canada ''wanaunga mkono hatua ya Harry na Meghan kuishi huko' lakini bado majadiliano zaidi yanahitaji kufanyika kuhusu hilo na gharama zilizopo''.
Aliongeza kwamba hadi wakati huu serikali ya Canada bado haijahusishwa kuhusu kile kitakachohitajika katika hatua ya wanandoa hao kuishi Canada.
Akizungumza katika kipindi cha Global News, kupitia Shirika la utangazaji la Canada, bado kuna maamuzi mengi ambayo yanastahili kufanywa na familia ya kifalme na wanandoa wenyewe kulingana na mapendeleo yao.
"Bila shaka tunaunga mkono hatua yao lakini pia kuna wajubu wa kufanywa vilevile."
Awali, katika mazungumzo yaliyofanyika Sandringham, ambayo yalihusisha Malkia, mwanamfalme wa Charles na William, yalikuwa yenye tija.
"Familia yangu na mimi tunaunga mkono uamuzi wa Harry na Meghan wa kuanza maisha mapya kama familia changa," amesema Malkia.
"Japo tungependa iwapo wangeendelea kutekeleza majukumu yao ya kifalme kikamilifu, tunaheshimu na kuelewa matakwa yao ya kuishi maisha ya kujitegemea kama familia wakiendelea kuwa sehemu muhimu ya familia yangu, Malkia amesema."
Aliongeza kwamba tumekubaliana kuwa watakuwa na kipindi cha mpito ambapo wawili hao wataishi Canada na Uingereza baada ya Harry and Meghan kuweka wazi kwamba hawataki kutegemea pesa za umma katika maisha yao mapya".
Mazungumzo ya dharura yalipangwa baada ya Harry na Meghan kutoa taarifa iliyoshangaza Familia ya Kifalme wiki iliyopita.
Pia walisema kuwa wanataka kuanza majukumu mapya na kujitegemea kifedha.
Miezi ya hivi karibuni, Harrry na Meghan walizungumzia changamoto za maisha ya kifalme na kuangaziwa zaidi katika vyombo vya habari huku mwanamfalme akisema kwamba anahofia mkewe huenda akakutana na yale ambayo mamake alikutana nayo ambayo yalisababisha kifo chake.
'Ni wazi kwamba Malkia anajutia uamuzi huu'
Hatua hii ni thabiti na isiyo rasmi na pia ni ya kibinafsi zaidi, Malkia amesma.
This is a remarkably candid and informal, almost personal, statement from the Queen.
Majuto kwa hatua ya Harry na Meghan yako wazi - angependelea iwapo wangesalia na majukumu yao ya sasa.
Lakini pia ameweka wazi kwamba wao bado ni watoto wa kifalme na kwamba wataendelea kuthaminiwa wakati wanaendelea kujitegemea.
Kuna maswali mengi yaliyoibuka kuhusu hatma ya maisha yao ya kifalme, husiano wao na wengine waliopo kwenye kasri, nani atakayelipia gharama na vile Harry na meghan watakavyojitegemea.
Kuna mengi ya kujadiliwa. Na siyo yote yatakayowekwa wazi kwa umma.
Na inaonekana kana kwamba Malkia anachukua hatua hii kama mchakati wala siyo kitu cha kufanyika kwa siku moja. Amezungumzia kipindi cha mpito wakati Harry na Meghan wanatumia muda wao Canada na Uingereza.
Malkia ametaka uamuzi ufanywe katika siku chache zijazo lakini huenda pia maamuzi yao yakapitiwa tena miezi au miaka ijayo.
Waziri wa Uingereza alipoulizwa na mwanahabari wa BBC Dan Walker kuhusu hatima ya Harry na Meghan katika Familia ya Kifalme amesema:
''Mtazamo wangu kuhusu hili uko wazi''. ''Mimi ni shabiki mkubwa bila shaka wa Malkia na Familia ya kifalme…ni kiungo muhimu sana katika nchi yetu.
Boris Johnson ameongeza: ''Nina Imani kwamba watatatua suala hili…lakini itakuwa vizuri iwapo sitazungumza lolote kuhusu hili