Mwanahabari anayehamasisha kuhusu Ebola ameuawa DR Congo

Wahudumu wa afya wakimzika mtoto wa miezi 11katika mkoa wa Kivu Kaskazini, nchini DRC, Mei 5, 2019.


Serikali nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na imelaani mauaji ya mwanahabari anayehamasisha kuhusu Ebola.
Katika taarifa ya pamoja ya wizara ya afya ya nchi hiyo kwa ushirikiano na mashirika ya ya kimataifa yanayohusika na mapambano dhidi ya ugonjwa hatari wa Ebola wamelaani vikali mashambulio yaliyofanyika usiku wa Jumamosi katika kijiji cha Lwemba mkoani Ituri kaskazini mashariki mwa DRC.
Wanajeshi wanasema waliwatambua washambuliaji waliovamia nyumba ya Papy Mumbere Mahamba katika kijiji cha Lwebma, eneo la Kaskazini mashariki mwa mkoa wa Ituri, na kumuua, kumjeruhi mke wake na kuteketeza moto nyumba yao.
Chanzo cha mauaji hayo bado hakijajulikana jap mamlaka za nchini humo imeanza uchunguzi kubaini ikiwa ilihusiana na mapambano dhidi ya Ebola.
Washukiwa wawili wanazuiliwa kuhusiana na mauaji hayo
DR Congo inashuhudia mlipuko hatari wa virusi hatari vya Ebola epidemic kwa mara ya pili.
Watu wanaofanya kazi ya kukabiliana na ebola mara kwa mara wanalengwa na nakubdi ya watu wanaopinga juhudi zao.
Mhariri wa BBC, Will Ross anasema katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita wahudumu kadhaa wa afya wameshambuliwa na watu wanaopinga kampeini ya kukomesha ebola.
Mahambulio hayo yanaaminiwa kuwa kuchochewa na imani ya watu wengi kwamba virusi vya ebola ni njama ya uwongo, hali ambayo imechangia watu kutowaamini watu wanaofanya kazi katika sekta ya afya.
Wataalamu wa afya wakiomba watu kukomesha matambiko ya jadi wakati wa mazishi ili kuhakikisha mtu hajiweki katika hatari ya maambukizi, kwa mfano huzua husababisha chuki.
Watu wengine hata wanafikiria hakuna Ebola na kwamba ni kitu kilichobuniwa na wataalamu wa matibabu ili wapate kazi za mishahara mikubwa.
Nini kilifanyika?
Bw. Mahamba alikuwa akiendesha kipindi cha kuhamasisha watu kuhusu katika kituo cha redio cha kijamii shambulio hilo lilipofanyika.
Profesa Steve Ahuka, mshirikishi wa kitaifa wa wa mapambano dhidi ya Ebola, alithibitisha ripoti kutoka kwa wanajeshi kuwa "mhudumu wa kijamii" aliyekuwa anajihusisha na mapambano dhidi ya Ebola.
Wanahabari katika kituo cha Redio cha Lwemba, alipokuwa nafanya kazi, pia wamethibitisha tukio hilo. Jacques Kamwina aliambia shirika la habari la AFP kwamba Mahamba alichomwa kisu hadi kufa.
Hali ya Ebola ikoje DRC?
Taifa hilo lilitangaza ugonjwa huo kuwa janga la kitaifa mwezi Agosti 2018. Zaidi ya watu 2,000 walifariki kutokana na ugonjwa huo huku visa vingine 3,000 vya maambukizi vikithibitishwa, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).
Mlipuko huo iliathiri zaidi mikoa ya Kivu Kaskazini,Kivu Kusini na Ituri.
Je inawezekana kuangamiza virusi vya Ebola?
Mwezi Julai, WHO: Mlipuko wa Ebola janga la dharura
Juhudi za kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo zimelemazwa na mashambulio dhidi ya wafanyikazi wa afya katika vituo vya kutoa huduma za matibabu.

Ebola ni nini?

  • Ebola ni ugonjwa unaoambukizwa na virusi ambapo aliyepata maambukizi hupata dalili za homa, uchovu, maumivu ya viungo na koo.
  • Kisha mgonjwa hutapika, kuharisha na kutoka damu.
  • Watu huambukizwa kwa njia ya kugusana, njia ya mdomo na pua, pia kwa njia ya damu, matapishi, kinyesi,majimaji ya kwenye mwili wa mtu mwenye Ebola
  • Wagonjwa hupoteza maisha kutokana na kupungukia maji mwilini na viungo kushindwa kufanya kazi.

Post a Comment

Previous Post Next Post