Wanamgambo wa kaskazini mashariki
mwa Mali wamewaua wanajeshi 49 katika shambulio lililotokea jeshini,
mkuu wa jeshi ameandika katika kurasa zake za Facebook.Katika kurasa ya twitter, jeshi limeelezea kuwa shambulio hilo ni la kigaidi.
Mali imekuwa ikikabiliana na vurugu za mara kwa mara tangu mwaka 2012, wakati ambao wanamgambo wa kiislamu waliposhambulia kaskazini mwa nchi hiyo.
Kwa msaada wa Ufaransa, jeshi la Mali lilikuwa linalinda usalama wa eneo hilo lakini bado vurugu zinaendelea.
Vurugu hizo imeenea hata katika mataifa mengine ya jirani.
Hakuna kikosi cha kigaidi ambacho kimekiri kuhusika na shambulio hilo katika maeneo ya Indelimane huko Menaka.
Mali pamoja na Burkina Faso, Chad, Niger na Mauritania - ni miongoni mwa nchi ambazo majeshi yao yanafadhiliwa na Ufaransa.
Vikosi vitano vya taifa vinashuku kuwa wajumbe wa Ansarul walishambulia mwezi septemba.
Kundi la Ansarul Islam, likimaanisha kuwa watetezi wa dini ya kiislamu, lilianzishwa mwaka 2016 na mhubiri maarufu Ibrahim Malam Dicko.
Mwaka 2012, iliripotiwa kuwa wanamgambo wa kiislamu kaskazini mwa Mali walishambulia eneo hilo
Tags
Kimataifa