
Mnamo mwaka 2016, alihukumiwa kifungo cha miaka 22 gerezani baada ya kukiri makosa 71 ya ubakaji wa watoto waliokuwa na umri wa miaka kati ya sita na 12 kati ya mwaka 2006 na 2014.
Inafahamika kuwa alishambuliwa siku ya jumapili alipokuwa katika mahabusu ya gereza la Full Sutton karibu na York, na kisu kinachotumiwa jikoni.
Katika kesi dhidi ya Huckle mwaka 2016 wapelelezi waliochunguza kpmpyuta yake walibaini zaidi ya picha na video zaidi ya 20,000 za aibu za matukio yake ya ulawiti wa watoto.
Alizishirikisha kwa walawiti wengine kote duniani kupitia wavuti wa siri uliofahamika kama wavuti wa giza.

Katika mwisho wa kesi yake , Judge Peter Rook alisema kuwa hukumu ya Huckle inaonyesha " kero la umma " kuhusu "kampeni yake ya ubakaji ".
Alisema "Ni nadra sana kwa jaji kumuhukumu mtu mmoja kwa makosa ya ubakaji kwa kiwango hiki ."

Alijitambulisha kama mkristo na kwamba alitembelea Malaysia kwa mara ya kwanza kama mwalimu alipokuwa na umri wa miaka 18 au 19.
Baadae alikuwa akiwasaidia watoto kukuza vibaji vyao huku akifanya kazi ya kujitolea.
Akielezea kumhusu mmoja wa waathiriwa wa unyanyasaji, alijisifu akisema "Nilimharibu msichana wa miaka 3 ambaye alikuwa amenipenda kama mbwa wangu na hakuna yeyote aliyejali ."
Mwaka jana BBC ilianda kipindi maalum kumuhusu Huckle, kilichofichua uhalifu wake miongoni mwa watoto nchini Cambodia, India na Uingereza
Tags
Kimataifa