Dalili za mimba

Admin
By -
0
Kwenye makala hii nakuonyesha dalili za mimba zote za mwanzo na zile za baada ya miezi miwili hivi.
Dalili na ishara za mwanzo za mimba
Si wanawake wote wanaziona na kupitia dalili za aina moja wanapokuwa wamepata mimba. Kila mmoja anaweza kupata dalili tofauti na mwingine.
Kwa kawaida mwanamke anaweza kuona dalili tofauti katika mimba ya kwanza na mimba nyingine zinazofuata baada ya hii ya kwanza.
Baadhi ya dalili za mwanzo kama kutokuona siku zako na kuongezeka uzito ni dalili zinazotokea karibu kwa wanawake wote na katika ujauzito za mwanzo na hata zinazofuata
Jina langu naitwa Fadhili Paulo. Endelea kusoma …
Pokea dondoo na makala nyingine mhimu kuhusu MATATIZO YA UZAZI kwa wanawake na wanaume kupitia WhatsApp BURE, ili kujiunga tuma neno > AFYA YA UZAZI likifuatiwa na jina lako na mahali ulipo kwenye WhatsApp +255714800175
Dalili za Mimba Changa
Dalili na ishara zingine za mwanzo za mimba ni pamoja na:
  • Mabadiliko ya kihisia
  • Kukojoa mara kwa mara
  • Kuumwa kichwa
  • Maumivu ya mgongo eneo la chini
  • Matiti kuuma
  • Chuchu kuwa nyeusi
  • Uchovu
  • Homa za asubuhi
Mimba ya miezi miwili
Baada ya miezi miwili mwanamke anaweza kuonyesha dalili zifuatazo za kuwa ni mjamzito;
  • Miguu kuvimba
  • Maumivu ya mgongo
  • Kiungulia
  • Kukojoa mara kwa mara
  • Kupata pumzi fupi fupi
Dalili za mimba changa huanza kuonekana baada ya muda gani?
Baadhi ya wanawake wanaweza kuziona dalili na ishara za mimba ndani ya wiki za mwanzo za mimba kutungwa wakati wengine wanaweza kuziona dalili hizo baadaye zaidi baada ya kuwa wamepata ujauzito.
Dalili za mimba za mwanzo zaweza kuonekana sawa na zile ishara za kupata hedhi ya kwanza na hivyo mwanamke anaweza asitambuwe ikiwa dalili anazoziona ni za mimba au ni za kutaka kupata siku zake.
Je dalili za mimba zinafanana kwa wanawake wote?
Dalili za mimba zaweza kuwa tofauti baina ya wanawake.
Dalili hizo za mimba baina ya wanawake zinaweza kutofautiana katika ubora na wingi wake na hata mwanamke mmoja anaweza kuonyesha dalili tofauti kwa kila mimba anayopata.
Dalili za mwanzo za mimba zinaweza pia kujitokeza au kuonekana katika vipindi tofauti wakati mwanamke akiwa mjamzito.
Kipimo kijulikanacho kama HCG (human chorionic gonadotropin ) hufanyika ili kubaini uwepo wa ujauzito kwa kutumia mkojo au damu. HCG ni homoni ambayo huzalishwa ya yai lililorutubishwa kutungwa katika kuta za mji wa uzazi.
Vipimo vya kisasa vya kutambua kutungwa kwa mimba vinaweza kuonyesha mwanamke kuwa amepata ujauzito hata kabla ya mwanamke kutoona siku zake.
Kipimo cha kutambua kutungwa kwa mimba kwa kutumia damu kinaweza kuonyesha mimba kutungwa mapema zaidi kuliko kipimo cha kutumia mkojo.
Kupitia makala hii nitakueleza kwa kina dalili za mimba za kawaida za mwanzo na zile zinazojionyesha katika hatua za mbele za kutungwa kwa ujauzito.
Kupanga kupata mimba
Kupanga kupata mimba kunahusisha majadiliano kati ya mme wa mwanamke anayetaka kupata ujauzito na timu ya wataalamu wa afya wa mke wake na kunahusu majadiliano yanayohusiana na chakula na lishe, mazoezi, maandalizi ya kisaikolojia na masharti juu ya vyakula na vinywaji vya kuvieupuka mama awapo mjamzito.
Baadhi ya wanawake kutokana na kuwa na mzunguko wa hedhi usioeleweka wanaweza kupata mimba na wasitambuwe mara moja kama ni wajawazito mpaka aina fulani maalumu za dalili za mimba zitakapoanza kujitokeza. Hili linaweza kusababisha mama kutumia vitu ambavyo hakutakiwa kutumia akiwa mjamzito kwakuwa hakuwa anajuwa wala kuonyesha dalili zozote kabla kuwa ni mjamzito.
Wanawake wanaochagua kuchukua muda na kupanga au kujiandaa maalumu kwa ajili ya kupata mimba wanakuwa na uwezo mkubwa wa kuepuka kutumia vyakula au vinywaji au kuishi aina ya maisha ambayo yanaweza kuwa hatari kwa ujauzito.
Dalili 16 za mimba changa
Hizi ni dalili 16 mwanamke anaweza kuziona mwanzoni mwa mimba kutungwa:
  1. Kutoona siku zake: Kutoona siku zake ndiyo dalili ya kwanza ya mwanamke kuhisi huenda amepata mimba. Na kawaida wakati wote wa ujauzito mwanamke hawezi kuona siku zake. Wakati mwingine dalili za kutungwa kwa mimba zinaweza kufanana na zile za kutaka kutokea kwa hedhi. Pia wanawake wenye mzunguko usioeleweka wanaweza wasitambuwe mara moja ikiwa wamepata ujauzito au la. Siyo jambo la kawaida kwa dalili za mimba kujitokeza kabla mwanamke hajaisi kukosa siku zake lakini ikiwa mwanamke ana mzunguko usioeleweka basi hili linaweza kutokea.
  2. Maumivu katika mji wa uzazi: Maumivu kiasi au hali ya kutokujisikia vizuri inaweza kujitokeza wakati yai lililorutubishwa linapojijenga katika kuta za mji wa uzazi siku 6 mpaka 12 za mwanzo za mimba kutungwa.
  3. Kujitokeza uchafu ukeni: Baadhi ya wanawake wanaweza kuona uchafu mzito kidogo kama maziwa ukitoka katika siku za mwanzo za ujauzito. Hili hutokea ndani ya wiki za mwanzo za ujauzito wakati kuta za uke zikiwa zinaongezeka ukubwa na unene. Uchafu huu unaweza kuendelea kutokea wakati wote wa ujauzito. Ikiwa uchafu huu unatoa harufu mbaya au unaambatana na maumivu inaweza kuwa ni maambukizi ya bakteria na ni mhimu kuonana na daktari haraka kwa uchunguzi na msaada zaidi.
  4. Maziwa kubadilika: Wanawake wengi wanashuhudia mabadiliko katika maziwa yao mwanzoni kabisa mwa wiki za kwanza za mimba kutungwa. Mabadiliko hayo ni pamoja na maziwa kuuma, kuwa malaini, mazito, yaliyojaa, na hisia za mchonyoto au msisimko. Mabadiliko haya kwa kawaida hupotea pole pole baada ya wiki kadhaa baadaye.
  5. Chuchu kuwa nyeusi: Chuchu ambalo ni sehemu ya mbele kabisa ya ziwa la mwanamke linaweza kubadilika rangi na kuwa jeusi zaidi.
  6. Uchovu: Ingawa dalili hii inawezekana isiwe ya ujauzito moja kwa moja hata hivyo wanawake wengi wanaripoti kujisikia uchovu ndani ya wiki za mwanzo za mimba kutungwa.
  7. Homa za asubuhi, kujisikia vibaya na kutapika: Hata hivyo hizi homa za asubuhi siyo lazima zitokee asubuhi tu, zinaweza kutokea wakati wowote katika siku iwe mchana au usiku. Baadhi ya wanawake hawakutani na homa hizi au usumbufu wa aina hii katika kipindi chao chote cha ujauzito wakati wengine huwa ni shida kubwa kipindi karibu chote cha ujauzito. Usumbufu huu kwa kawaida hutokea wiki la pili mpaka la nane tangu ushike mimba na usumbufu huu unaweza kupotea wenyewe kuanzia wiki la 13 mpaka la 18.
  8. Kukerwa na baadhi ya harufu: Baadhi ya harufu zinaweza kumkera kirahisi mjamzito na hata kupelekea kutokujisikia vizuri na hata kutapika mwanzoni mwanzoni mwa ujauzito wake.
  9. Kukojoa mara kwa mara: Kuanzia wiki ya 6 mpaka ya 8 baadhi ya wanawake wanaweza kutokewa kupata mkojo mara kwa mara sababu ya mabadiliko katika homoni zao kutokana na ujauzito. Ikiwa dalili zingine zinajitokeza kama maumivu wakati wa kukojoa unatakiwa kuonana na daktari haraka kuona ikiwa una maambukizi kwenye mfumo wa mkojo (U.T.I) au la.
  10. Kizunguzungu au udhaifu: Hili pengine linaweza kuwa ni matokeo ya mabadiliko ya homoni ambayo yanaahiri pia usawa wa sukari katika damu, au kama matokeo ya shinikizo la damu.
  11. Kufunga choo: Mabadiliko ya usawa wa homoni yanaweza kupelekea baadhi ya wanawake kupata tatizo la kukosa au kufunga au kupata choo kigumu kinachoweza kuleta ugonjwa wa bawasiri mwanzoni mwa wiki za kwanza kwanza za ujauzito.
  12. Kuumwa kichwa: Maumivu ya kichwa au kuumwa kichwa kunaweza kuwa ni dalili za mimba katika wiki za mwanzo na maumivu haya yanaweza kuwa yanaletwa kutokana na mabadiliko ya homoni katika mwili na wakati mwingine yanaweza kutokea kama matokeo ya kufunga choo au kupata choo kigumu na kuna baadhi ya wanawake wanaweza kupata maumivu haya katika kipindi chote cha ujauzito wao.
  13. Kupenda aina fulani ya vyakula: Mwanamke anaweza kutengeneza aina nyingine ya hamu ya vyakula vingine ambavyo hakuwa anavipenda sana kabla ya ujauzito. Hii hali inaweza kudumu katka kipindi chote cha ujauzito. Wakati mwingine anaweza kupenda vyakula ambavyo hata haieleweki kama vile kula udongo au limau mara kwa mara.
  14. Maumivu ya nyuma ya mgongo: Hii mara nyingi hutokea wiki za mbele zaidi tangu upate ujauzito. Maumivu nyuma ya mgongo kwa chini yanaweza kutokea mwanzoni kabisa unaposhika ujauzito. Maumivu haya yanaweza kuja kupotea wakati wote wa kipindi cha ujauzito.
  15. Kubadilika kwa hisia: Kubadilika badilika kwa hisia za mwanamke ni dalili mojawapo za mimba wiki za kwanza na mara nyingi ni matokeo ya mabadiliko katika homoni zake. Mabadiliko haya pia yanaweza kuletwa na msongo wa mawazo (stress) au sababu zingine.
  16. Pumzi fupi: Baada ya mimba kutungwa mahitaji ya oksijeni kwa mama huongezeka zaidi ili kusapoti afya ya kiumbe kipya tumboni. Hili linaweza kusababisha baadhi ya wanawake kupatwa na tatizo la pumzi fupi dalili zinazofanana na pumu.
Dalili za mimba ya miezi miwili
Dalili nyingi za mwanzo za mimba zinaweza kuendelea mapaka miezi 6 au miezi mitatu ya mwisho. Dalili hizo ni pamoja na zifuatazo;
  • Kubadilika kwa hisia
  • Kuumwa kichwa
  • Kukojoa mara kwa mara
  • Maumivu ya nyuma ya mgongo
  • Kupenda aina fulani ya vyakula
  • Uchovu
Baadhi ya dalili kama maziwa kuwa malaini na kujisikia vibaya hupotea zenyewe kadri mimba inavyozidi kukua.
Wakati huo huo dalili za ujauzito wa miezi miwili zina uhusiano na kuongezeka kwa ukubwa wa mji wa uzazi na kuongezeka kwa uzito wa mwili kati ya miezi mitatu mpaka sita ya ujauzito na wakati mwingine mpaka wakati wa kujifungua.
Siyo wanawake wote wanakutana na dalili hizi kama zilivyo na uzito ulio sawa.
Dalili 7 za mimba ya miezi miwili
  1. Kuongezeka uzito: Wanawake wengi wanaweza kuongezeka uzito wa kilogram 11 mpaka 15 wakati wa ujauzito. Uzito kuongezeka ni matokeo ya kukua kwa mtoto tumboni, kitovu, maziwa kuongezeka na kuongezeka kwa ujazo wa damu na maji. Tabibu au nesi wako wa karibu atakuwa akirekodi na kufuatilia uzito wako kila mara.
  2. Maziwa kubadilika: Maziwa ya mwanamke yataongezeka kidogo kidogo wakati wote wa ujauzito mpaka anajifungua. Wakati mwingine maziwa yanaweza kujitokea tu hata kabla ya kuanza kunyonyesha.
  3. Kiungulia: Shinikizo kutoka katika mji uliongezeka wa uzazi hupelekea utumbo kusogezwa kidogo kwa juu tofauti na eneo lake la mara zaote na hili ndilo linalosababisha kutokea kwa kiungulia. Mabadiliko ya homoni piayanaweza kusababisha hili.
  4. Miguu kuvimba: Presha kutoka kwenye kuongezeka kwa mfuko wa uzazi inaweza kupunguza kiasi cha damu inayotiririka kwenda miguuni na hivyo kupelekea maji maji kujirundika miguuni na kutengeneza uvimbe.
  5. Kuvimba Veni: Kuongezeka kwa ujazo wa damu kunaweza kuleta tatizo la kuvimba kwa veni na ugonjwa wa bawasiri.
  6. Kukojoa mara kwa mara: Presha ya mji wa uzazi inaongeza presha nyingine kwenye kibofu cha mkojo na kusabbaisha hali ya kukojoa mara kwa mara. Wakati mwingine mwanamke anaweza kuona mkojo unatoka wakati akicheka, akikohoa au hata akipiga chafya.
  7. Pumzi fupi: Kuongezeka kwa ukubwa wa mji wa uzazi kunaisukuma diaphragm juu kuelekea kifuani na hivyo kusababisha upate pumzi fupi fupi tofauti na ulivyokuwa kabla ya ujauzito.
Vitu vya kufanya ili kupunguza dalili zisizo nzuri za mimba
Zipo baadhi ya dawa za asili, dawa lishe na matunzo maalumu binafsi yanayoweza kusaidia kupunguza au kuondoa maudhi haya ya wakati wa ujauzito.
Dawa nyingi hata antibiotiki zinaweza kutumika na mjamzito lakini mjamzito asitumie dawa yoyote iwe ya asili au ya hospitali bila ruhusa au uangalizi wa karibu wa Tabibu.
Unaweza kufanya yafuatayo ili kupunguza maudhi hayo;
  • Mlo sahihi na mazoezi ya viungo. Mlo sahihi na mazoezi ya viungo vinaweza kusaidia kudhibiti uzito. Usifanye kila aina ya mazoezi unayoyafahamu, wasiliana na Tabibu wako wa karibu kwa ushauri zaidi juu ya mazoezi gani hasa yatakufaa.
  • Usikae kwenye kiti au chini masaa mengi, bora kutembea tembea au kulala kuliko kuwa kwenye kiti masaa yote.
  • Vaa viatu vya kawaida na siyo vyenye visigino virefu au vinavyobana sana
  • Usilale kwenye godoro linalobonyea kirahisi
  • Vaa sidiria kubwa inayoaacha maziwa kwa uhuru wote
  • Kula zaidi vyakula vyenye nyuzi nyuzi (fiber) ili kuepuka kupata choo kigumu na bawasiri. Hii inamaanisha asilimia 80 ya chakula iwe ni matunda na mboga za majani.  
  • Kula milo mingi midogo midogo ili kupunguza kujisikia vibaya na kiungulia. Epuka vyakula vyenye mafuta sana. Kunywa mara nyingi maji na juisi za matunda za nyumbani.
Dalili za Mimba na dalili za siku zako
Dalili nyingi za mwanzo za mimba zinafafanana sana na dalili za mwanzo za kutaka kupata siku zako.
Mpaka utakapoona siku zako zimeanza au kipimo cha ujauzito kinaonyesha ni mjamzito hakuna njia inayoweza kuhitimisha ikiwa dalili unazoziona ni za ujauzito au ni za kupata siku zako.
Pokea dondoo na makala nyingine mhimu kuhusu MATATIZO YA UZAZI kwa wanawake na wanaume kupitia WhatsApp BURE, ili kujiunga tuma neno > AFYA YA UZAZI likifuatiwa na jina lako na mahali ulipo kwenye WhatsApp +255714800175
Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)