Daktari apagawa kukutana na mtoto mwenye moyo ulio upande wa kulia

Admin
By -
0


Dodoma. Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) imemgundua mtoto wa kiume (15) mwenye moyo ulio upande wa kulia, kitu ambacho si cha kawaida kwa kuwa moyo huwa upande wa kushoto.
Ingawa watu wa aina hiyo wapo, daktari aliyebaini suala hilo, Wilfredius Rutahoire amesema ameshtushwa kukutana kwa mara ya kwanza na mtu mwenye moyo upande wa kulia.
“Tangu nianze kazi ya udaktari sijawahi kukutana na mtu ambaye moyo wake uko upande wa kulia,” amesema Rutahoire, ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo katika Hospitali ya BMH.
“Hali hiyo ilinilazimu kuwasiliana na baadhi ya madaktari wengine wa moyo kama waliwahi kuona mtu mwenye moyo upande wa kulia ambao nao waliniambia hawajawahi.”
Amesema mtoto huyo, ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sababu za kimaadili, aligundulika wakati wa utekelezaji wa huduma mkoba (medical outreach) iliyofanyika Wilaya ya Kondoa kwa siku tatu kuanzia Julai 15, 2019 ikiwa na lengo la kuwafikia watu wenye matatizo ya moyo.
Kwa habari zaidi soma gazeti la Mwananchi la leo Jumatano Julai 24, 2019

Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)