
Dadashev mwenye umri wa miaka 28, alishindwa kuendelea na pambano hilo ambalo mkufunzi wake, Buddy McGirt, alilazimisha lisimamishwe katika raundi ya 11 baada ya bondia huyo kupokea kichapo kikali.
Pambano hilo lilipigwa Julai 20, 2019, ambapo baada ya pambano Dadashev alikimbizwa hospitali na madaktari walimfanyia vipimo na kugundua kuwa damu ilikuwa ikimvuja kwenye ubongo na kufanyiwa operesheni ya saa mbili, ambapo jana Jumanne alipoteza maisha.
Tags
Michezo