ZARI AMJIA JUU DIAMOND

Admin
By -
0
MZAZI mwenza wa mwanamuziki Diamond Platnumz,  Zari Boss Lady,  amefunguka baada ya msanii Diamond kuongea mengi kuhusu mahusiano yao yaliyopita ndani ya kituo chake cha redio cha Wasafi FM jana,  April 23, 2019.

Diamond alifunguka mambo mengi ikiwemo Zari kum-cheat kwenye mahusiano, kuhusiana na kutoa sapoti kwa wanaye, na mambo mengine yaliyokuwa yanawahusu walipokuwa kwenye mahusiano.

Majibu ya Zari yalitoka rasmi wakati Diamond akiwa live kwenye mahojiano ambayo yalikuwa yanaruka moja kwa moja  kwenye mitandao ya kijamii, radio na televisheni.

Zari alituma video tatu kwenye akaunti yake ya Instagram zilizokuwa na maelezo yanayosomeka:  “Sasa yale magoti mpaka Sauzi yalikuwa ya nini? Kule  kuomba msamaha kwote kwa radio kwa nini? Kwani umekuwa comedian sasa? Usinichafulie maisha bro. Yameisha zamani kubali tu. Kiki zimekuwa ngumu mjini. Niheshimu tafadhali nakulelea watoto tena vizuri”.


Video ya kwanza Zari amelalamikia kushushiwa heshima na kusema kwamba Diamond anajitetea kwa kumsingizia kwamba alikuwa na mahusiano mengine wakati bado wakiwa pamoja.


Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)